GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Ukiwaacha JWTZ, ni taasisi ipi ya uma raia wa kawaida ana imani kuwa atatendewa haki bila kuinunua?
1. Polisi?
Wengine wanasema kuingia kituo cha Polisi ni bure lakini kutoka ni hela
2. Mahakama?
Malalamiko ni mengi kuwa hata watafsiri Sheria nao baadhi yao si wasafi
3. TRA?
Inasemekana ni mabingwa wa kutengeneza mazingira ya kuhongwa
4. Trafiki?
Kuna mwaka nilikodi gari la mizigo kunibebea mizigo fulani kutoka Chalinze hadi Arusha. Tuliposimamishwa Moshi, Askari aliusogelea mlango wa dereva na kusema, tena kwa sauti kabisa: "Fanya shala au nikague".
Alipopewq chochote akaruhusu gari liondoke bila hata kuuliza kama dereva ana leseni au la
5. Idara ya ardhi?
Humo kuna uozo usioelezeka
6. Hospitali?
Sina uhakika kwa sasa, lakini kipindi cha Magufuli, zilianza kujirekebisha
7. Bunge?
Inasemekana nalo wakati mwingine linahongwa
8. Magereza?
Huko ni kama ulimwengu mwingine. Vilio vya wanaoonewa vinaishia humo humo. Hakuna anayesikia kilimo chao
9. Idara ya maliasili?
Inasemekana kuna raia wengi waliouwa baada ya kukutwa kwenye maeneo yanayodaiwa ni ya hifadhi. Badala ya kufikishwa kwenye vyombo vya Kisheria, wahusika waliamua kumalizana nao kwa kuwamaliza.
10. Uhamiaji?
Majibu yanajulikana!
11. Bandari?
Kuna kipindi hata Serikali nayo ililakamika kuwa inapigwa
12. Tume ya uchaguzi?
Labda kuanzia sasa ni tofauti na miaka mingine
Itakuwa heri kama hayo hapo juu ni uongo.
Lakini kama ni ya kweli, inaashiria nini? Uonevu na rushwa ni sehemu ya maisha ya Watanzania? Zimehalalishwa kisirisiri?