SoC02 Uongo mtamu ni kupika matokeo ya ukweli wenye uchungu

SoC02 Uongo mtamu ni kupika matokeo ya ukweli wenye uchungu

Stories of Change - 2022 Competition

CHE_BUEVARA

Member
Joined
Aug 11, 2021
Posts
5
Reaction score
3
Nakusalimu kwa lugha ya Kiswahili na vyovyote utakavyonijibu ni sawa tuu. Hahaha! Hebu kumbuka ulivyokua mtoto zile ‘kamba’ wazee wako walikua wanakupiga? Sasa kuna hii moja ambayo nadhani kila mzazi amewahi kuitumia kwa mtoto/watoto wake na hao watoto pia wanaendelea kuitumia kwa watoto wao.

Jamani nyie eti ukipata Mdogo wako ukimuuliza mama kampata wapi anakwambia “NIMEMNUNUA” Hahaha basi hapo unakuta na wewe unalazimisha wakununulie wa kwako pia na waliokua na uwezo wakawazawadia ‘midoli’na bado shida haikuishia hapo wanataka kama yule wa mama.

Kuna ile tabia ya watoto kukataa kula labda, unakuta mzazi anamwambia mtoto usipokula naita dudu akumeze basi hapo mtoto woga juu, kinyonge atajitahidi kula. Kimsingi ni njia zilitumika kuwahadaa watoto ili jambo jema lifanyike lakini kama wazazi tunajiandaaje kuusema ukweli pale utakapohitajika? Kwasababu hawa watoto hawatobaki watoto milele, kuna siku watayafikia tuu hayo mambo tuliyowalisha ‘matango pori’.

Haya sasa nadhani umeona namna malezi yetu yalivyojaa vificho hata kwenye vitu ambavyo ni muhimu kuvijua tangu tukiwa wadogo kabisa na hapo nadhani ndipo shida ya kutokua na mazungumzo ya wazi baina ya watoto na wazazi huanzia. Hebu fikiria alipokua mtoto ulimwambia Mdogo wake mmemnunua na leo kakua sasa, unaanzaje kumwambia namna alivyopatikana ili yeye katika umri wake hasa kipindi cha balehe asije pata huyo mtoto?

Na wewe unawaza utamwambiaje mtoto wa miaka mitatu ukweli kuhusu upatikanaji wa mtoto eh? Sasa hapo naomba urudi darasa la nne/tano pale kwa sie tuliosoma mtaala wa kitanzania tulianza kujifunza ile mada ya ‘Reproduction’ kwa ufupi sana halafu wakatuambia kujifunza Zaidi subiri ufike darasa la sita. Haha sasa pale walituweza hata wasiopenda shule walijitahidi kusubiri ili waione inakuaje ile kitu bwana.

Ninachojaribu kusema hapa ni kutafuta njia nzuri isiyo ya uongo wala kificho kulingana na umri wa mtoto maana huwezi kumbebesha mzigo asioweza kuutua.

Kimsingi kwenye huu uongo na kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu kama hayo ya uzazi, lishe na mengineyo ndio tunapotengeneza kizazi kisichokua na udadisi kabisa yaani wanakua wale wale wa kutaka vitu rahisi ili maisha yaendelee. Hebu fikiria ungemwambia huyu Mdogo wako ni matokeo ya uumbaji wa Mungu kwa wale waamini sasa, bila shaka dogo lazima atauliza kama sio Mungu ni nani basi uumbaji ni nini na hapo mzazi unampa madini ambayo mtoto anakua na uwezo mkubwa wa kuuliza kwa udadisi Zaidi na Zaidi. Hata umri ukifika sasa unakua hupati ukakasi kuendelea na ‘dozi’ ilipoishia ili kumpa kile kinachomfaa.

Matatizo mengi tunayokutana nayo sasa ni matokeo ya upuuzi mwingi tuliouchukulia kawaida kwa miaka mingi. Siku hizi kila nyumba yenye binti wa miaka 20 kama hajazalia nyumbani basi ukifatilia sana ameshachoropoa mimba hata tatu tayari. Haya ni mambo ambayo tungeanza nayo chini hata tusingekua tunajadili hili tatizo la mimba za utotoni au hata vijana wadogo kuwa ndio wahanga wakubwa wa magonjwa hatari ya zinaa.

Kuna namna huwa tunakwepa mazungumzo ya uwazi juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa kimvuli cha heshima pamoja na maadili ya jamii Fulani lakini ukweli ni kwamba, umri wa balehe na ngono ni vitu visivyopishana hata kidogo na matokeo yake huwa ni mimba na magonjwa wakati mwingine ambayo hayajifichi. Wataalamu wanasema hakuna mtihani mgumu kuushinda kama hitaji la kufanya jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako. Sasa tujiulize, ukitoa pesa inayokuaga inawasha mfukoni Je ngono si moja ya mtihani huo?

Kuna jamaa mmoja mtaani kwetu hakuwa sawa kiakili kwa mtazamo wa jamii yetu pale basi mama mmoja wa makamo akasema huyu hana shida mbona, mpeni mke tuu mtanipa matokeo. Haha! Nilicheka sana japo sikuelewa sana lakini naamini wewe umeshasikia mambo haya pia.

Watanzania tumejaaliwa misemo, nahau, methali na vingine vingi ambayo tungevifanyia kazi ipasavyo tungekua na kizazi ‘amazing’ sana na leo tujaribu kukumbushana kulingana na hili tunaloongea leo.

Samaki mkunje angali mbichi, hata tusiwaze kwa ugumu sana hapa maana yake wale watoto tungewaandaa na taarifa sahihi kuhusu afya ya uzazi leo hii tusingehangaika kujiuliza tunamalizaje tatizo la mimba za utotoni.

Mbuyu ulianza kama mchicha, kirahisi tuu jamani hawa watoto wanakua na kuwaficha kunafanya tatizo nalo lizidi kukua kadri liwezavyo.

Ukiona mwenzako ananyolewa, zako tia maji. Bado tatizo wazazi walikua wanaliona na hawakuchukua njia bora za kuwaandaa watoto wao ili nao wasiwe wahanga wa tatizo badala yake tukawajaza woga wa kuuliza na uongo usio na maana sana.

Ngoja ngoja, yaumiza tumbo, najua wengine hudhani watoto ni wadogo sana wanasubiri akua akue lakini ukweli ni kwamba kila umri na ‘dozi’ yake bwana hivyo ukisubiri tatizo linakua kubwa na kulitatua ni mtihani mno.

Usione vyaelea, vimeundwa. Kitu chochote kizuri na maadili yakiwemo ndani yake huwa kuna gharama yake ya kufikia hapo hivyo lazima na sisi kama wazazi wajao tuanze kuwaunda watoto wetu mapema ili kuvunja mduara wa uzushi.

Asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu. Usiombe walimwengu wakufunzie mtoto wako tena wa kike. Hahaha, muandae kijana wako kwasababu huo ulimwengu sio salama kwa ajili yake kujifunza vitu vya muhimu kama afya ya uzazi.

Kwa kumalizia tuu, hata ndugu zetu waumini wa dini ya kikristo wanaweza kutusaidia ule mstari unaozungumzia kumfundisha mtoto njia impasayo nae hatoiacha hadi atakapofikia uzee. Tujitahidi kuwaeleza ‘ukweri’ hahaha, wakiamua ujinga inakua ni wao na sio kukosa taarifa sahihi ndio kumfanye afanye ujinga wake. Tuendelee ku’tozoka.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom