Uongozi Mzuri ni Upi wa kuchaguliwa na wananchi au kuteuliwa?

Uongozi Mzuri ni Upi wa kuchaguliwa na wananchi au kuteuliwa?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Nimekuwa nikijiuliza Kuwa Viongozi wote walioteuliwa wana furaha kweli au Ndio huogopa hata kucheka.

Mbona kama wanaishi maisha ya hofu sana Jamani maana kama mkeka ukisoma Jina halipo hiyo nayo ni shida nyingine.

Wanapaswa kuishi vipi hawa watu ili wawe na furaha na wafanye kazi kwa ufanisi?

Mtu kwenye hotuba yake yote ni ya kumshukuru na kumsifia mteuzi, point chache. hii itakuwa hadi lini?

Viongozi wa kuchaguliwa na wananchi nao wana shida zao Jamani.

Sijui wanataka kuongoza kwa miaka mingapi?

Wataenda kutetemekea wajumbe, vikao vya usiku haviishi yani ni shida.

Kwani haiwezekani mtu wa kawaida kuongoza?

Mtu hajawai leta maendeleo lakini anataka tu kuwa kiongozi muda wote Jamani wapeni nafasi na wanaoweza msiwapoteze.

Kuchaguliwa au kuteuliwa?
 
Uongozi mzuri ni nidhamu, weledi, uadilifu na uwajibikaji. Mengine yote ni viawini tu (accessories).
 
Back
Top Bottom