LGE2024 Uongozi wa CCM Dodoma wafanya vikao mfululizo Kujiweka sawa Uchaguzi serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301


Uongozi wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini chini ya Mwenyekiti Charles Mamba umeendelea na mikutano ya mfufulizo na mabalozi wote 2000 wa Jimbo la Dodoma Mjini katika kujiweka sawa kuelekea katika uchaguzi wa serikali wa mitaa ambapo leo kikao kimefanyika cha Mabalozi kutoka Kata ya Makutupora, Chihanga, Ipala, Chahwa, Hombolo Makulu na Hombolo Bwawani.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa CCM wilaya *Ndg. Charles Mamba amewapongeza Mabalozi kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya na kuwataka kuhimiza wanaCCM kushiriki kwa wingi katika Uchaguzi huo.


Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewapongeza mabalozi kwa kazi nzuri waliyofanya ya uhamasishaji wananchi kujiandikisha katika daftari la wakazi na kuwataka kufanya kazi nzuri kuwahamasisha wananchi wengi zaidi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo wa serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27.11.2024

Mkutano huo ulienda sambamba na ugawaji wa vitendea kazi kwa mabalozi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-11-09 at 17.51.22.jpeg
    103.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-09 at 17.51.23 (1).jpeg
    91.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-09 at 17.51.25.jpeg
    171.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-09 at 17.51.25 (1).jpeg
    168.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-11-09 at 17.51.26 (1).jpeg
    116.5 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…