Uchaguzi 2020 Uongozi wa CHADEMA ulikuwa sahihi "kuwatimua" TBC katika uzinduzi wa kampeni zake

Uchaguzi 2020 Uongozi wa CHADEMA ulikuwa sahihi "kuwatimua" TBC katika uzinduzi wa kampeni zake

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Nianze mada yangu kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 18(1) nayo inasema hivi "Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi na pia uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati na mtu yeyote" mwisho wa kunukuu.

Hebu sasa tutazame nini kilitokea kule Zakheim Mbagala katika ufunguzi wa kampeni zake chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA.

Watangazaji wa TBC walifika "kwa shingo upande" katika uwanja huo kwa nia ya kuonyesha LIVE matangazo hayo.

Nini kilitokea katika urushaji matangazo hayo?

Wasikilizaji wa TBC walibaini kukatwa katwa kwa matangazo kwa matangazo hayo.

Ndipo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa alipoamuru watangazaji hao "wafungashe virago" vyao na waondoke uwanjani hapo katika muda wa dakika 15!

Wapo wananchi wanawalaumu viongozi wa CHADEMA kuwa eti kitendo chao hicho kilikuwa si cha kiungwana!

Hapo hapo TBC wakatoa taarifa ya kulaani kitendo cha kufukuzwa "kinyama" watangazaji wake kwenye ufunguzi wa kampeni hizo.

Hebu turejee katika utangazaji wa TBC katika kipindi chote hiki cha utawala wa serikali ya awamu ya 5, bila shaka hata mtoto mdogo anayesoma chekechea atakuwa anajua kuwa TBC imejigeuza kuwa kama televisheni ya CCM, kwa kutangaza "sifa na mapambio" kwa serikali hii ya CCM, chini ya kiongozi wake Rais John Magufuli.

Hata hivyo TBC ni chombo cha Umma na hakipaswi "kuhodhiwa" na chama chochote cha siasa na kinapaswa kitoe "airtime" iliyo sawa kwa vyama vyovyote vya siasa nchini, bila kufanya upendeleo wowote, kwa kuwa sisi wananchi walipa kodi, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, ndiyo tunaoiendesha TBC

Nini kilitokea jana?

Ni dhahiri kuwa hao TBC walifika pale uwanjani Zakheim kwa maelekezo maalum ya wakubwa wao ili waje "wauhujumu" ufunguzi huo wa kampeni.

Nimesikiliza tamko lao TBC la kulaani "kutimuliwa" pale uwanjani, wakihalalisha ukatajikataji wao wa matangazo, wakidai wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2020, ya maudhui ya vyombo vya habari!

Niwaukize TBC hivi mnajua kuwa sheria mama, nikimaanisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiyo "supreme" ya sheria zote nchini?

Kwa kuweka ibara ya sheria iliyoko kwenye Katiba, hamuoni kuwa nyinyi TBC ndiyo mmeivunja Katiba ya nchi kwa kutotaka wananchi waisikie hotuba ya viongozi wakuu wa ChADEMA kwa kisingizio cha sheria yenu kandamizi ya vyombo vya habari, ambayo "inajicontradict" na sheria mama, ambayo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatoa Uhuru huo wa habari haupaswi uingiliwe kati na chombo chochote hapa nchini?
 
TBC walienda kupiga story zao kwenye mikutano ya CHADEMA. kuita Live ilikua ni njia ya kupiga per diems.
Haijawahi tokea duniani eti unafanya narration na analysis kwenye tukio Live.

TBC hawana tofauti na Njugushi kwa walichokua wanakifanya. Wanasimulia watu tukio ambalo watu wenyewe wanaliona Live.
 
Aibu kubwa sana kwa TBC
Hivi inawezekanaje TBC ndiyo ijifanye inafanya "censorship" ya matangazo wanayoyarusha na kukatakata matangazo, wakidai kuwa maudhui yake hayaendani na maudhui ya sheria ya vyombo vya habari?

Kinachokatazwa kwenye sheria hiyo ni matusi pekee

Hebu TBC muueleze Umma wa watanzania ni sehemu gani katika hotuba ya viongozi wa CHADEMA jana walitukana?

Hivi kwa viongozi wa CHADEMA kuishinikiza Tume ya Taifa ya uchaguzi kurejesha majina ya wagombea wa vyama vya upinzani, ambayo yamekatwa kihuni ndiyo kulisababisha TBC iyakate kate matangazo hayo?

Hivi nini kina maslahi kwa Taifa letu, Tume iyakate kihuni majina hayo au viongozi wa upinzani waishinikize Tume hiyo ili itende haki kwa kuwarejesha hao walioenguliwa kihuni?
 
Hii inaonyesha taswira mbaya iliyojengwa na watawala ,upendeleo,uonevu Sheria mbaya zenye kukidhi maslahi yao Tena zinapitishwa kwa miswaada ya hati za dharura. Tusiyakubali haha yanatuharibia taifa letu.
 
Tutaona leo kama watakuwa wanakata ili kukidhi sheria ya maudhui
Thubutu yao?

Hata wakiona Mwenyekiti wao akiwatukana wazi wazi viongozi wa upinzani, hawatathubutu kuyakata matangazo hayo!
 
Mystery usichokijua tu ni kwamba hata hao TBC walihisi na walifanya 'Kusudi' ili 'muwatimue' na wapate sababu. Kiufupi Wao ndiyo Washindi hapa.
Uko sahihi hapo kwamba walienda ili watkmuliwe wapate sababu na wamepata sababu. Lakini kwa majority ya watanzania wanaojielewa wanajua janja yao hata kabla walipotangaza watarusha matangazo kila mtu alijua haikuwa bure.

So I think it's win win and lose lose situation.

TBC: wamepata walichotaka, ila mbele ya macho ya watu wametoa ushahidi wa rangi yao halisi
CHADEMA: Wamepata huruma kwa kuonekana wanahujumiwa, lakini Wamekosa coverage.
 
Hii inaonyesha taswira mbaya iliyojengwa na watawala ,upendeleo,uonevu Sheria mbaya zenye kukidhi maslahi yao Tena zinapitishwa kwa miswaada ya hati za dharura.Tusiyakubali haha yanatuharibia taifa letu.
Yaani hao wabunge wa Ndiyoo, ipite hiyo sheria.

Ndiyo wanaolisababashia Taifa hili linaangamia!
 
Kuna watu wamezoea kulaumu Kila kitu,mpaka kwenye kupewa haki yake mtu analaumu, tutaendelea kutoa stahiki zote Kwa wagombea wote wa vyama vyote Kwa usawa ili wa Tanzania wapiga kura watambue ni yupi na Nani ana wafaa kuleta maendeleo na yupi ataleta vurugu na maandamano yasiyo na msingi
 
CDM wamewekewa mtego na sasa wameingia kichwa kichwa, hii inamaanisha hakuna mkutano wa CDM katika kampeni za 2020 utakaokuwa live tena, TBC walikuwa wanatafuta sababu tu na kweli mmewapatia justification.

Kwa Tz ni watu wangapi wana uwezo kuangalia mkutano wote kwa live streaming online, ukijumlisha na changamoto za ubora wa internet kwa streaming kwa maeneo mengi Tz, unapata jibu moja tu, CDM wameshawekwa kibra, kinachofuata kinajulikana.
 
CDM wamewekewa mtego na sasa wameingia kichwa kichwa, hii inamaanisha hakuna mkutano wa CDM katika kampeni za 2020 utakaokuwa live tena, TBC walikuwa wanatafuta sababu tu na kweli mmewapatia justification.

Kwa Tz ni watu wangapi wana uwezo kuangalia mkutano wote kwa live streaming online, ukijumlisha na changamoto za ubora wa internet kwa streaming kwa maeneo mengi Tz, unapata jibu moja tu, CDM wameshawekwa kibra, kinachofuata kinajulikana.
Kwa bahati nzuri hata wewe kada unakiri kuwa hao TBC wanawatumikia nyinyi tu!

Hiyo inathibitisha na kuonyesha namna hao watangazaji walivyo mashabiki wa kindakindaki wa CCM!

Hata hivyo usisahau kuwa hao ni televisheni ya Taifa na wanapaswa wawe "fair" katika utangazaji wao, kwa kuwa chombo chao kinaendeshwa kwa kodi zetu wananchi wa Taifa hili, bila kujali itikadi zetu za kisiasa
 
Back
Top Bottom