Watakapo kata matangazo ya mungu wao huko Dodoma Leo mm natembea uchi kutoka temeke mpaka sinzaTutaona leo kama watakuwa wanakata matangazo ili kukidhi matakwa ya sheria ya maudhui
Nakubaliana na wewe kabisa. Hao jamaa walikuwa wanatafuta sababu tu ya beef na CDM liwe rasmi. Hiyo TV huwa inachefua sana na sidhani kama inatazamwa na watu wawanaojielewaMystery usichokijua tu ni kwamba hata hao TBC walihisi na walifanya 'Kusudi' ili 'muwatimue' na wapate sababu. Kiufupi Wao ndiyo Washindi hapa.
Wanaingizwaga chaka kiboya sanaMystery usichokijua tu ni kwamba hata hao TBC walihisi na walifanya 'Kusudi' ili 'muwatimue' na wapate sababu. Kiufupi Wao ndiyo Washindi hapa.
Mnawaonea Watangazaji bur, wao huwa hawajui ukifanya nini unakosea....anayejua yupo huko juu hivyo wanachofanya wao ni kubahatisha tu kwamba hili ni kosa na hili ndio sahihi.Hivi inawezekanaje TBC ndiyo ijifanye inafanya "censorship" ya matangazo wanayoyarusha na kukatakata matangazo, wakidai kuwa maudhui yake hayaendani na maudhui ya sheria ya vyombo vya habari?
Kinachokatazwa kwenye sheria hiyo ni matusi pekee
Hebu TBC muueleze Umma wa watanzania ni sehemu gani katika hotuba ya viongozi wa CHADEMA jana walitukana?
Hivi kwa viongozi wa CHADEMA kuishinikiza Tume ya Taifa ya uchaguzi kurejesha majina ya wagombea wa vyama vya upinzani, ambayo yamekatwa kihuni ndiyo kulisababisha TBC iyakate kate matangazo hayo?
Hivi nini kina maslahi kwa Taifa letu, Tume iyakate kihuni majina hayo au viongozi wa upinzani waishinikize Tume hiyo ili itende haki kwa kuwarejesha hao walioenguliwa kihuni?
Hakuna mtego hapo, kwanza tbccm haiangaliwi na watu wengi sana kama huna habari.CDM wamewekewa mtego na sasa wameingia kichwa kichwa, hii inamaanisha hakuna mkutano wa CDM katika kampeni za 2020 utakaokuwa live tena, TBC walikuwa wanatafuta sababu tu na kweli mmewapatia justification.
Kwa Tz ni watu wangapi wana uwezo kuangalia mkutano wote kwa live streaming online, ukijumlisha na changamoto za ubora wa internet kwa streaming kwa maeneo mengi Tz, unapata jibu moja tu, CDM wameshawekwa kibra, kinachofuata kinajulikana.
Nami niliwaza hivyo ila nkasema ngoja muda utaamuaMystery usichokijua tu ni kwamba hata hao TBC walihisi na walifanya 'Kusudi' ili 'muwatimue' na wapate sababu. Kiufupi Wao ndiyo Washindi hapa.
Tutaona leo kama watakuwa wanakata matangazo ili kukidhi matakwa ya sheria ya maudhui
Swali hapa kutokana na hoja yako, "Kwanini TBC iwaingize chaka CDM"?Wanaingizwaga chaka kiboya sana
Hivi hawa TBC watajisikiaje hapo Oktoba 28, watakapoona Mheshimiwa Tundu Lissu ndiye katangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu?Hakuna mtego hapo,kwanza tbccm haiangaliwi na watu wengi sana kama huna habari.
Wapuuzi sana, kodi zetu zitawatokea puani
Siasa ni mchezo mchafuSwali hapa kutokana na hoja yako, "Kwanini TBC iwaingize chaka CDM"?
Suala ni kuwa hiko chombo cha habari cha TBC kinaendeshwa kwa kodi zetu sote wana-ccm na wana Chadema, sasa swali la kujiuliza ni kwa vipi wao wajifanye kama chombo cha habari cha chama kimoja tu cha CCM?Mimi nimeshangaa kwamba kumbe TBC inafuatiliwa Sana kiasi kwamba wana CDM walilalamikia kwamba matangazo yalikua yanakatakata.
Nikawaza Kama yanakatakata TBC si nikuangalia kupitia njia nyingine na kuwaacha TBC ili kila mmoja atumie uhuru wake.
Wanaosema huwa hawaangalii TBC unawakuta ndio wnaolalamika ilikua inakatakata.
Makosa ya TBC hayakusahihishwa kwa hekima na kutumiwa vyema na CDM zaidi waliharibu zaidi na kiki ikahamia kwa TBC sio kwa uzinduzi wa kampeni.
Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Mystery usichokijua tu ni kwamba hata hao TBC walihisi na walifanya 'Kusudi' ili 'muwatimue' na wapate sababu. Kiufupi Wao ndiyo Washindi hapa.
TBC ni hovyo kabisa na inaudhi!Nianze mada yangu kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 18(1) nayo inasema hivi "Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi na pia uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati na mtu yeyote" mwisho wa kunukuu.
Hebu sasa tutazame nini kilitokea kule Zakheim Mbagala katika ufunguzi wa kampeni zake chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA.
Watangazaji wa TBC walifika "kwa shingo upande" katika uwanja huo kwa nia ya kuonyesha LIVE matangazo hayo.
Nini kilitokea katika urushaji matangazo hayo?
Wasikilizaji wa TBC walibaini kukatwa katwa kwa matangazo kwa matangazo hayo.
Ndipo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa alipoamuru watangazaji hao "wafungashe virago" vyao na waondoke uwanjani hapo katika muda wa dakika 15!
Wapo wananchi wanawalaumu viongozi wa CHADEMA kuwa eti kitendo chao hicho kilikuwa si cha kiungwana!
Hapo hapo TBC wakatoa taarifa ya kulaani kitendo cha kufukuzwa "kinyama" watangazaji wake kwenye ufunguzi wa kampeni hizo.
Hebu turejee katika utangazaji wa TBC katika kipindi chote hiki cha utawala wa serikali ya awamu ya 5, bila shaka hata mtoto mdogo anayesoma chekechea atakuwa anajua kuwa TBC imejigeuza kuwa kama televisheni ya CCM, kwa kutangaza "sifa na mapambio" kwa serikali hii ya CCM, chini ya kiongozi wake Rais John Magufuli.
Hata hivyo TBC ni chombo cha Umma na hakipaswi "kuhodhiwa" na chama chochote cha siasa na kinapaswa kitoe "airtime" iliyo sawa kwa vyama vyovyote vya siasa nchini, bila kufanya upendeleo wowote, kwa kuwa sisi wananchi walipa kodi, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, ndiyo tunaoiendesha TBC
Nini kilitokea jana?
Ni dhahiri kuwa hao TBC walifika pale uwanjani Zakheim kwa maelekezo maalum ya wakubwa wao ili waje "wauhujumu" ufunguzi huo wa kampeni.
Nimesikiliza tamko lao TBC la kulaani "kutimuliwa" pale uwanjani, wakihalalisha ukatajikataji wao wa matangazo, wakidai wanafanya hivyo kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2020, ya maudhui ya vyombo vya habari!
Niwaukize TBC hivi mnajua kuwa sheria mama, nikimaanisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndiyo "supreme" ya sheria zote nchini?
Kwa kuweka ibara ya sheria iliyoko kwenye Katiba, hamuoni kuwa nyinyi TBC ndiyo mmeivunja Katiba ya nchi kwa kutotaka wananchi waisikie hotuba ya viongozi wakuu wa ChADEMA kwa kisingizio cha sheria yenu kandamizi ya vyombo vya habari, ambayo "inajicontradict" na sheria mama, ambayo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inatoa Uhuru huo wa habari haupaswi uingiliwe kati na chombo chochote hapa nchini?