Uongozi wa Chriss Brown uko tayari kufanya kazi na Ali Kiba

Joined
May 5, 2015
Posts
34
Reaction score
67
Uongozi wa muziki nchini marekani unao muongoza msanii wa R&B Chris Brown umetoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unao muongoza msanii kutoka Tanzania ALI KIBA msanii ambae yupo chini ya uongozi wa Kampuni za SAMSUNG.

Kwa taarifa zilizopo katika mtandao wa VIP Beats nchini marekani zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014 uongozi wa msanii Chris Brown ulipokea maombi ya muungano wa wasanii wawili kufanya wimbo wa pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris Brown maombi hayo yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za msanii Ali kiba ikiwemo SINGLE BOY, MWANA pamoja na wimbo aliofanya katika project ya ONE 8.

Uongozi wa Chris Brown umethibitisha kupokea taarifa za maombi hayo na umeonesha kupenda sauti ya msanii Ali kiba na kutoa tamko kua wapo tayari kusimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na wasanii hawa.

Upande wa msanii Chris Brown amesema hana tatizo yupo tayari kushirikiana na msanii Ali kiba kwani alipata nafasi ya kutazama project ya One 8 na ameona kiwango cha msanii Ali kiba kinaridhisha japokua anahitaji marekebisho madogo sana.
 
Nimesikia CASH MONEY BROTHERS wanataka kumsajili msanii DUDUBAYA kwenye label yao aisee.
 
Reactions: ora
Capture sehemu walio kubali tujiridhishe maana binafsi siwaamini wote mpaka Mond, mmekuwa waongo waongo sana, hayo ndio mazara ya kutembea na yule bibi bomba maana mmerithi uongo uongo wa Bongo movie. Mwenzio jana kasema kanunua nyumba SA, ununue nyumba SA unakaa madale? Inaingia akilini? Wewe eti Kiba na Criss Brown, wakati kolabo na Davido hatujui hatima yake!! kwani mmekula maharage ya wapi nyie watu? Mtuache basi kidogo.. Msipo weka evidance nanyela mumo mumo. Pambavu zangu kabisa.
 
mond amesikia??asije akamuwahi mwenzie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…