Uongozi wa chuo kikuu sauti waendesha ufisadi wa kutisha kwa wanafunzi wake

Fighter G

Member
Joined
Oct 8, 2011
Posts
17
Reaction score
4
UONGOZI WA CHUO KIKUU SAUT WAENDESHA UFISADI WA KUTISHA KWA WANAFUNZI WAKE

UTANGULIZI

Uongozi wa juu wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (Main Campus – Mwanza) umendesha ufisadi wa hali ya juu kwa wanafunzi wake kwa kumtumia aliyekuwa mwajiriwa ofisi ya uhasibu (Oditing) Ndugu Stephen Maurice Deya (31) ambaye alitumiwa kukusanya ada za wanafunzi ambazo zinakisiwa kuwa Zaidi ya Millioni Mia saba kinyume cha utaratibu halafu baadae wanafunzi hao wakageukwa na uongozi wa chuo na kutakiwa kulipa ada zao upya (Double payment) kitu kilichosababisha wanafunzi wengi kushindwa kulipa hivyo kukatisha masomo yao huku Ndugu Stephen Maurice Deya akiachiwa huru bila kufunguliwa Mashitaka yoyote.

NAMNA UFISADI ULIVYOENDESHWA

Imezoeleka kwamba ada na malipo mengine ya chuo SAUT hufanyika Bank ya CRDB na NBC, lakini toka Ndugu Stephen Maurice Deya aajiriwe 2009 mfumo mpya wa ulipaji ada Cash dirishani ukaanza, Ndugu Deya aliwatangazia wanafunzi kwamba kutokana na foleni za bank kuwa kubwa wanafunzi wanaruhusiwa kulipa pesa zao cash dirishani kwake na kupewa risiti, lakini wengine waliambiwa kuwa Ndugu Deya amepewa kazi maalum ya kushughulikia malipo ya wanafunzi wanaokidai chuo. (Wanafunzi wanaokidai chuo niwale ambao hulipiwa na makampuni ya madini na kampuni nyinginezo ambao inasemekana wakati mwingine hulipa pesa nyingi zaidi kwa chuo kuliko kiwango ambacho mwanafunzi anadaiwa hivyo mwanafunzi anakuwa na haki ya kudai pesa iliyozidi, Pia kuna wanafunzi ambao wamelipa pesa zao binafsi kwa chuo halafu baadae Bord ya mikopo ikawalipia tena na hawa pia hulazimika kudai pesa yao iliyozidi). Kwahiyo Ndugu Deya alionekana amepewa task ya kukusanya fedha cash ili hao wanaokidai chuo waweze kurejeshewa in cash kwasababu chuo hakikuwa tayari kuandika cheque kwa kila anayekidai kwani pesa zingine zilikuwa ni ndogo tu.

Kutokana na hali hiyo ndugu Deya aliwatumia viongozi wa serikali ya wanafunzi na viongozi wa Kanisa na wanafunzi wengine katika kuhakikisha kwamba zoezi hili linafanikiwa, kwahiyo viongozi hao wakawa wanawaelekeza watu kuhusu utaratibu huo na kuwezesha watu walipe ada zao kwa njia rahisi kupitia Maurice kwani ni kweli kwamba miezi ya kulipa ada foleni huwa ndefu sana, wengine waliwapokea wanafunzi wa mwaka wa kwanza na kwenda kuwalipia kwake bila kujua kwamba mchakato huo ulikuwa batili uliosukwa na uongozi wa chuo, mamia ya wanafunzi wakalipiwa kwa mtindo huo, wakapewa risiti halisi kutoka ofisi ya uhabu na wakaendelea na masomo na mitihani yao kama kawaida.

KWANINI WATU WALIMUAMINI STEPHEN MAURICE DEYA

Katika hali ya kawaida mtu anaweza akashangaa kwani nini mamia ya wanafunzi waamue kumwamini Ndg. Deya na kumkabidhi fedha zao bila wasiwasi wowote. Ukweli ni kwamba ndugu Deya alijengwa na kutengenezewa uaminifu wa hali ya juu katika jamii ya SAUT, kazi ya kumjenga hivyo ilifanywa na baadhi ya viongozi wa juu wa chuo wakiongozwa na Makamu mkuu wa chuo Rev. Dr. Charles Kitima.

STEPHEN MAURICE DEYA ALIVYOJENGWA NA KUWEKWA KWENYE SYSTEM HII YA UFISADI

Stepen Maurice Deya alisoma Advanced Diploma ya Uhasibu katika chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino 2007 – 2009, muda wake mwingi aliutumia kufanya shughuli za kanisa kwani alikuwa kiongozi wa kanisa kama mnavyojua SAUT ni chuo ambacho kipo chini ya Baraza la maaskofu wakatoliki Ndugu Deya alikuwa kiongozi wa halmashauri hapo kanisani akionekana kuwa karibu sana na uongozi wa juu wa chuo. Kwa bahati mbaya Ndugu. Deya hakufanikiwa kumaliza chuo mwaka 2009 kutokana na kufeli somo moja, alikosa mark moja tu, makamu mkuu wa chuo Rev. Dr. Charles Kitima akaagiza mtihani wake huo aliofeli usahihishwe upya kwa hisia kuwa huenda Ndugu. Deya ameonewa au amefeliswa makusudi (Jaribu kuangalia intervention hii ya makamu mkuu wa chuo kwa kijana huyu, kwasababu kimsingi Ndugu Deya alitakiwa kucomplain mwenyewe na si mkuu wa chuo kuingilia kati jambo dogo kama hili ambalo huwa linawatokea mamia ya wanafunzi na huwa haingilii) kilichotokea baada ya mtihani wa Deya kusahishwa upya majibu yakaja vilevile kwamba amefeli akapata marks 49 kama alizopata mwanzo, Hivyo hakugraduate.

Pamoja na Ndugu Deya kukosa sifa za kugraduate bado uongozi wa juu wa chuo uliendelea kumbeba labda ni kwasababu ya kujua kuwa walikuwa wamemwandaa kutekeleza mkakati maalum.

YAFUATAYO YALIFANYIKA ILI KUENDELEA KUMJENGA NDUGU STEPHEN MAURICE DEYA LICHA YA KUSHINDWA KUMALIZA CHUO:

1. Uongozi wa chuo ulimwajiri Ndugu Stephen Maurice Deya mwaka huo huo moja kwa moja kwenye ofisi ya uhasibu, hakuna mchakato wowote rasmi ambao ndugu Deya alipitia, tukamuna tu anaanza kufanya kazi ofisi ya uhasibu akiwa amepewa Baraka za uongozi wa juu. (Tumezowea kuona chuo hiki SAUT kikiwabakiza wanafunzi waliofauru vizuri kama wafanyakazi au kuwapa fursa ya kuendelea kusoma ngazi ya juu zaidi lakini kwa Deya ilikuwa tofauti kwani alipewa direct imployment akiwa si tu hajafauru vizuri bali ameshindwa kabisa kugraduate.

2. Ndugu Deya alirudia mtihani wake aliofeli akiwa mfanyakazi wa SAUT, imagine mwajiriwa ofisi nyeti ya uhasibu anakwenda kurudia mtihani mmoja na wanafunzi anaowahudumia, alifanikiwa kufaulu mtihani huo na aliendelea kuwa kiongozi anayeaminika kazini kutokana na wakuu walivyokuwa wakimproud.

3. Ilipofika 2010 Stephen Maurice Deya akiwa na 28 years wakati huo aliruhusiwa na uongozi wa chuo kugombea Ubunge wa jimbo la Nyamagana kupitia CCM akitokea ofisini japokuwa aliambiwa agombee kupitia CHADEMA akagoma, alifanikiwa kushiki kampeni zote katika mchakato wa kura za maoni CCM, Alitumia pesa nyingi sana kama mnavyojua mabo ya siasa lakini uongozi uliendelea kumpa support lakini kwa bahati mbaya akashindwa kwenye kura hizo za maoni. (Rejea majina ya waliocukua fomu za kugombea ubunge CCM Nyamagana).

4. Baada ya uchaguzi kwisha Rais, wabunge na madiwani walipokwisha kuchaguliwa bado chuo kilimtuma Stephen Maurice Deya kwenda kugombea nafasi ya uspika wa bunge la jamuuri ya muungano wa Tanzania akitokea ofisini, pamoja na kutumia hela nyingi tena bado nako alishindwa kupata nafasi hiyo kwasababu baada ya kufika Dodoma waliambiwa kuwa nafasi hiyo ya uspika ilikuwa ni zamu ya wanawake, (Rejea majina ya waliocukua fomu za kugombea Uspika wa bunge kupitia CCM)

5. Stephen Maurice Deya alipewa fursa ya kuendelea kusoma mpaka atakapochoka, hivyo kwa kipindi akiwa ofisini alikuwa mfanyakazi mwanafunzi ambapo alifanikiwa kumaliza post graduate mwaka 2011 na akaunganisha masters (ambayo hakuimaliza kutokana na kadhia hii) huenda ulikuwa mpango maalum pia kwani Kujichanganya kwake na wanafunzi kulimpa fursa kubwa zaidi ya kutekeleza mpango wa ufisadi kwani wanafunzi wenzake wengi walimpatia pesa akawaletea risiti.

6. Ilikuwa ni desturi ya Makamu mkuu wa Chuo kumsifia Stephen Maurice Deya kwenye makundi ya watu hasa kanisani na madarasani alipenda kumuita “Kijana wangu”, akipongeza hatua yake ya kugombea ubunge, uspika na jinsi kijana huyo alivyo mwaminifu na makini katika kazi.

7. Stephen Maurice Deya alikuwa na urafiki mkubwa sana na Mapadri, masista na watu wengine muhimu chuoni wakati huo amewaingiza wadogo zake pia katika uongozi wa kanisa, kimsingi alikuwa anaonekana ni mtu mwema na wakuaminika. Ilifika wakati ilianzishwa jumuiya mpya katika mtaa aliokuwa anaishi Stephen Maurice Deya maeneo ya kijiweni kwa masista jumuia hiyo ikaitwa kwa jina lake “Jumuia ya Mtakatifu Maurice” still existing to date.

Kutokana na sababu hizo hapo juu na nyingine nyingi Maurice Deya aliaminika kupita kiasi kwani kila alichikifanya kilionekana kusapotiwa na uongozi wa juu wa chuo ndio maana ilikuwa raisi kwake kukusanya fedha za wanafunzi kwani uongozi ulishamtengenezea njia, lakini pia risiti halisi za electroniki za chuo zilikuwa zinatolewa hapo hapo dirishani bila shaka yoyote, hakukuwa na utofauti kati ya risiti ya mtu aliyelipia bank na akabadilisha pay in sleep yake na kupata receipt ya chuo na Yule aliyelipa direct dirishani kwa Maurice. Wengi waliotumiwa na Maurice katika kutekeleza mpango huu na wakapata matatizo ni viongozi wa kanisa, viongozi wa serikali ya wanafunzi na waumini wazuri wakatoliki ambao Maurice alikuwa na sauti kwao kwani walikuwa wakimfahamu Maurice kwa sifa kemkem alizokuwa akipewa na viongozi wa juu wa chuo kiasi cha kutoweza kutilia shaka chochote kitakachofanywa na Stephen Maurice Deya.

SIRI YA UFISADI NA USALITI DHIDI YA WANAFUNZI ILIFICHUKA NA KUUMIZA WANAFUNZI FROM MAY 2012 TO DATE .

Mwanzoni mwa mwezi Mei 2012 tulishangaa kuona ndugu Stephen Maurice Deya akija kuchukuliwa na polisi kwa madai kuwa alikuwa akiwakatia wanafunzi risiti kinyume na utaratibu, tulishangaa kwasababu utaratibu huo ulikuwa ukifanyika pale ofisini na ulionekana kama kitu cha kawaida. Baada ya kukamatwa alipelekwa police station kituo cha Igogo Mwanza ambapo alikaa ndani siku tatu baadae akaachiwa.
Chuoni zikaanza kusakwa risiti zote zilizokatwa na Maurice kwa semester ile majina zaidi ya 130 ya wanafunzi yakabainika kulipa kwa mtindo huo, chuo kikawaamuru wote waliolipa kwa mtindo huo kulipa karo zao upya huku wale wanafunzi zaidi ya 20 ambao walikuwa wanawalipia au kuwaelekeza wenzao kwa Maurice wakiitwa kwenye kamati ya nidhamu ya chuo na kuhojiwa ambapo wapo waliofukuzwa chuo, wapo waliozuiliwa kufanya mitihani na wapo waliosamehewa.

Kitu cha ajabu hapa ni kwamba hawa wanafunzi waliotumiwa na mwajiriwa wa chuo ndugu Deya ndio walisulubiwa na kujengewa picha mbaya zaidi na kuonekana kana kwamba wao ndio waliokula karo za wanafunzi wenzao kitu kilichopelekea baadhi yao kuwekwa ndani na wengine kushindwa kabisa kufanya mitihani ilhali chuo kinafahamu ukweli kwamba hawa jamaa walikuwa wanatekeleza agizo la mfanyakazi wa chuo, lakini pia kiliwaumiza wanafunzi wengine kwa kuwataka walipe karo zao upya ilhali walishalipa na risiti halali za chuo wanazo. Ndugu Stephen Maurice Deya adhabu pekee aliyopewa ni kukaa ndani siku tatu na kuondolewa kazini, hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa dhidi yake hii inadhihirisha kuwa mpango huu ulikuwa ni wa viongozi wa chuo kwani katika kufanya ufisadi mkubwa kama huu tungetegemea mshtakiwa namba moja ambaye ni Ndugu, Deya afunguliwe mashtaka ya kukiibia chuo na si kurudisha mpira huu kwa wanafunzi.

KINACHOENDELEA HIVI SASA HAPA SAUT

Tulidhani jambo lile limekwisha kwa wanafunzi wale waliopita kulipishwa karo upya, lakini kinachoendelea sasa ni kwamba wanakagua risiti za wanafunzi wakikuta risiti yoyote iliyosainiwa na Deya iwe imelipiwa Bank au la wanamtaka mwanafunzi husika kulipa karo upya la sivyo watamzuwia kufanya mitihani au watamfukuza chuo kitu ambacho kimechanganya wanafunzi wengi chuoni hapa na kuwafanya wengine wakate tama ya kuendelea na kusoma kwasababu hawana uwezo wa kulipa pesa hizo upya na wanamuona mitaani mhasibu waliyemkabidhi fedha zao akiwa huru na anafanya shughuli zake kama kawaida.

KWANINI NASEMA UONGOZI WA CHUO UMEHUSIKA

1. Uongozi wa chuo umemwachia huru bila kumchukulia hatua yoyote mtu aliyekihujumu chuo zaidi ya 700 milioni ambaye ni Stephen Maurice Deya, hatua hii inadhibitisha kwamba huenda Deya alikuwa akikabidhi mapato hayo kwa wakuu hao na ndio maana wameshindwa kumchukulia hatua kwani ni kitu ambacho walikipanga wenyewe.

2. Stephen Maurice Deya alijengewa taswira nzuri kwenye macho ya watu na uongozi wa juu wenyewe kama nilivyoeleza hapo juu, kulikuwa na mkakati maalum wa kumuandaa kutekeleza kazi hiyo.

3. Taasisi kama SAUT inafanya Auditing kila mwaka, inakuwaje leo wanaanza kuwadai watu kulipa upya fedha za mwaka mmoja mpaka mitatu nyuma inamaana auditing yao wanayoifanya kila mwaka ilikuwa ni gereha tuu? Kwanini haikugundua wizi huu ambao ulianza tangu mwaka 2009?

4. Uongozi wa chuo umewabana wanafunzi waliolipa fedha kwa Maurice bila kuwapa ufafanuzi wa nini kinaendelea dhidi ya Maurice wanawanyanyasa wanafunzi kwasababu hawajui haki zao hivyo wanafunzi wanaogopa kureact kwa hofu ya kufukuzwa chuo.

Ni dhahiri kuwa vigogo wa chuo hiki wanaufahamu vizuri mpango huu, lakini wanajificha nyuma ya migongo ya watu wengine.

Hivi sasa kuna wanafunzi wengine wengi tu ambao wiki mbili kabla ya mtihani wameambiwa walipe upya karo zao za miaka ya nyuma kwasababu walilipa kwa mfumo huo wa Risiti halali toka kwa Maurice, hivyo kuna hatari ya wanafunzi hao kukosa mitihani yao inayotarajiwa kuanza tarehe 28 mwezi huu kwasababu hali ya uchumi ni ngumu.

Nimeamua kuliweka wazi hili baada ya kulifanyia utafiti wa kina, uzalendo umenishinda kwani nawaona watoto wakilia hovyo kwa kukosa matumaini wanapokuja ofisi ya uhasibu na kuambiwa kwamba wamekatiwa risiti feki, kama ni risiti feki waliwezaje kufanya mitiani yao previously? Kwanini chuo kisiendeshe kesi dhidi wizi huu kwa maslahi ya wanafunzi badala yake inawabebesha mzigo ambao hauwahusu? Kwasababu hapa chuo kimeibiwa na Maurice Deya lakini wao wanataka wizi wa Maurice ulipwe na wanafunzi what a shame?

WITO WANGU KWA WAZAZI NA WALEZI AMBAO WATOTO WAO WAMEATHIRIWA NA UFISADI HUU

Naomba msiwahisi vibaya watoto wenu kwamba wamekula karo au la bali hali halisi ndio hiyo niliyoieleza hapo juu, si kwamba waliathirika ni wajinga la hasha kuna uwezekano mkubwa kuwa chuo kilipanga tukio hili. Tuungane pamoja kulifikisha jambo hili kwenye vyombo vya sheria.

WITO WANGU KWA WANAFUNZI WALIOATHIRIWA NA MCHAKATO HUU

Tunzeni risiti zenu zote zilizokataliwa na chuo kwa kigezo kuwa hazikulipiwa bank huenda zikawa msaada mkubwa sana kwenu siku chache zijazo, Wapo baadhi ya wanafunzi na wazazi walioamua kulifuatilia jambo hili kisheria.

WITO WANGU KWA WATANZANIA, WANAHARAKATI NA WAPENDA MAENDELEO

Nawaomba watanzania wenzangu ifike mahali tusaidiane kupiga vita michezo kama hii ambayo kimsingi inawaumiza sana watanzania hasa masikini, ni dhahiri kwamba katika swala hili uongozi wa chuo umehusika kuwahujumu wanachuo lakini bado uongozi huo huo unataka kutafuta sifa ya kwamba ulifanikiwa kurejesha pesa zilizopotea kwa njia ya kuwakamua watanzania masikini ilhali wao wenyewe ndio waliokula pesa hizo. Tufuatilie swala ili kwa undani kwa manufaa ya vijana wote wa nchi hii, leo SAUT kesho litajitokeza sehemu nyingine.

Please share this info wasije watu wengine wakaibiwa tena kwa mpango huu au mwingine unaofanana na huu.

Kama unahabari nyingine muhimu kuhusu tukio hili tuinbox
1Share
Wazalendo Watata
January 21

11Share

3 people like this.
View 5 more comments
Daud Masingija wazalendo W.,Hata IFM ilbid wafnge barabara &kwa maandamano ndo serkal ina gutuka..ina kerasana 2popa1
January 21 at 10:45pm via mobile
Wazalendo Watata Kinachotusikitisha ni kwamba hiki ni chuo kinachomilikiwa na wanadini, hatukutarajia unyonyaji wa namna hii hawa jamaa mwaka jana wamepandisha pernat ya watu waliochelewa kulipa ada toka 10,000/= hadi 100,000/= yaani 1000% ilhali wanafahamu kuwa wanatoa huduma kwa watoto wa wakulima.
January 21 at 10:55pm · 1
Daud Masingija Wacha walvuruge lichuo lao,kama wataendelea kupata intake 'massive' syo monopolists vyuo vpokbao wawaulize META-MBEYA!
January 21 at 11:58pm via mobile
Maria Songo Aieseeeee
January 29 at 11:38pm
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom