Ngwanakilala
JF-Expert Member
- Jun 25, 2011
- 774
- 1,464
Wakale walisema actions speaks louder than words. Kwa matendo yake, over the last 10 years, it is obvious to everyone kuwa kuwa Falsafa ya Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, na serikali yake ya awamu ya nne ni ile ya OMBAOMBA. Bwana Kikwete anaamini katika omba omba mpaka aliwahi kutetea falsafa hiyo kwa kusema kuwa yeye ni baba na huwa anaondoka nyumbani kila wakati kwenda nje kuhemea ili atuletee watoto (watanzania) fedha za matumizi. Sasa je wachambuzi wabobezi wanasema nini kuhusu falsafa ya Ombaomba?
Kila mtu anaelewa kuwa omba omba huwa haheshimiwi.
Hata wale waungwana ambao kwao ni kawaida kutoa sadaka kila mara, huwa hawawaheshimu ombaomba. Ombaomba hawaheshimiki kwa sababu moja tu, kwamba wanaishi kwa kutegemea fadhila za watu wengine.
Hali inakuwa mbaya zaidi inapokuwa ombaomba anaonekana ni mtu anayeweza kufanya kazi na kujipatia kipato, lakini hafanyi kazi kwa sababu anaona kazi ni ngumu zaidi kuliko kuzurura akikinga bakuli.
Wafadhili wanaotupa misaada wanatushangaa kama sisi wenyewe tunavyowashangaa ombaomba wanaoonekana kuwa na viungo na akili timamu. Rasilimali tulizojaliwa kuwa nazo zinatosha kabisa kutuwezesha kujitegemea iwapo tungezitumia vizuri.
Badala yake tunaona ni rahisi zaidi kuwaachia wageni wachukue rasilimali zetu waende kuzifanyia kazi za kuwanufaisha wao, halafu sisi tuletewe makombo kama misaada. Hapa kuna kitu kimetusibu katika uwezo wetu wa kufikiri, kama vile tumeingiliwa na ‘virus' katika bongo zetu, na ndiyo maana tunafanya mambo ambayo hayaingii akilini.
Nimewahi kutoa mfano wa tumbili tunaowaona kandokando ya njia katika mbuga ya Mikumi. Wanatoka msituni ambako kuna matunda mengi na yenye ubora wa upya (kwa maana ya ‘fresh') kuja kushinda barabarani wakisubiri watalii wawarushie maganda mabovu ya ndizi zilizonyauka.
Ndivyo tulivyo, na wahisani hawatuheshimu kwa sababu hatuheshimiki. Kila kitu tunataka tufanyiwe na wengine, hata pale ambapo ni dhahiri kwamba tunaweza kujifanyia sisi wenyewe.
Tuambizane ukweli. Ni kwamba wanatuona sisi ni sawa kabisa na nyani. Dharau waliyonayo kwetu inazidi pale tunapopewa ‘misaada' kwa masharti fulani, na hayo masharti tunayakubali haraka haraka, lakini tukiisha kukabidhiwa ‘misaada' hiyo tunayasahau yale masharti na kufanya tunavyotaka.
Suala la kuheshimu makubaliano tuliyoyatilia saini ni muhimu mno. Ndipo tunapata tofauti kati ya muungwana na mhuni. Mhuni atatia saini waraka wowote, (bila hata kuusoma) alimradi kuna kitu anakitaka sasa hivi, lakini katika dhamira yake hana nia ya kuheshimu chochote kilicho ndani ya waraka huo. Akiisha kupata anachohitaji, anaweza wala asiuangalie huo mkataba tena.
Muungwana huheshimu makubaliano aliyoingia na wenzake, na katika kila hatua za utekelezaji ataurejea mkataba huo mara kwa mara kuhakikisha haendi kinyume cha makubaliano. Huo ndio uungwana. Ukiisha kuvunja makubaliano yako na ‘mfadhili' kwa kulipeleka gari la ‘msaada' kule ulikokatazwa, unakuwa umejiweka mahali pa kukemewa na mama ambaye alikwisha kutuona kama watu wa hovyo.
Tulipopata uhuru tukaamua kujenga taifa moja kutokana na mipaka ya utumwa wetu, lakini tumefika katikati ya safari tumesahau tulikuwa tunakwenda wapi, na tunachofanya sasa ni kukimbia katika mduara tukifuata mikia yetu: Tulikotoka hatuko tena, na tulikokusudia kwenda hatukumbuki ni wapi. Sasa tunagawana mbao za mashua yetu.
Sasa tumekuwa kama watu waliotekwa kiakili ambao hawawezi kufurukuta katika jambo lolote. Kama hatuna hata lugha tunayoweza kuiita na kuifanya kuwa lugha ya taifa, hatuwezi kujiita taifa. Kuiita lugha ya taifa ni jambo rahisi; tulikwisha kufanya hivyo, na tumefanya hivyo kwa muda wa miongo mitano. Lakini si kweli kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa. Ni kama vile ambavyo tumekuwa tukisema kwa miongo minne kwamba Dodoma ndio mji mkuu wa Tanzania wakati tukijua kwamba hilo nalo si kweli. Kila mtu anajua kwamba akitaka makao makuu ya serikali yafanye jambo fulani inabidi aende Dar es Salaam, na kama wahusika wako Dodoma kwa sababu ya kikao cha Bunge, atawasubiri warudi.
Ugumu wa kukubali ukweli katika hili, na hususan kwa watu wanaoiona lugha ya kigeni kama yenye hadhi ya utukufu kuliko lugha yao wenyewe umekuwapo kila mahali duniani. Lakini vile vile, inapotokea kwamba jamii inayojitambua kama taifa, hata kama ni taifa dogo, ikajihisi kwamba lugha yao inahujumiwa, jamii hiyo itachukua hatua za kupambana dhidi ya hujuma hizo, wakati mwingine kwa kumwaga damu.
Ikifikia hatua hiyo, jamii hiyo inakuwa na haki ya kujitambulisha kama taifa, na wakati mwingine utaifa huo unaweza ukawa hauna nchi, hauna ardhi ulipojisimika, lakini utaifa unadumu ndani ya nyoyo za watu wake, kokote kule waliko, hata kama wamesambaa na kutapakaa duniani kote.
Sisi hatuko hivyo.
By Jenerali Ulimwengu
Raiamwema Toleo 396
March 11, 2015