Uongozi wa Simba SC umechangia pakubwa Simba SC kudondosha point 2 dhidi ya Namungo FC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Nilishangazwa kuona timu anakabidhiwa Daniel Cadena ambaye ni kocha wa makipa wakati Kuna kocha mbobevu na mwenye uzoefu mkubwa katika michuano ya ndani na kimataifa si mwingine ni kochaJuma Mgunda.

inakuache kocha wa Makipa anakabidhiwa timu?!

Nini kipo nyuma ya pazia mpaka kocha Juma Mgunda anaachwa na kutopewa timu Ina maana viongozi wamesahau mchango wa Juma Mgunda ndani ya Simba sc !?

Kwa Simba sc kudondosha point mbili muhimu dhidi ya Namungo Fc wakulaumiwa ni viongozi na si vingine.

Tukubal tukatae Juma Mgunda Ni moja ya makocha wazuri wazawa ndani ya ligi yetu.

 
Huwezi kujua inawezekana alikataa, kupokea timu ikiwa haina team work na hawapo sawa kisaikolojia inahitaji moyo maana yeye pia anaangalia CV yake.

Lakini najiuliza kwanini viongozi wa Simba wanamwamini zaidi Matola kuwepo kwenye benchi la ufundi mbona ashawahi kuachiwa timu kwa mda na uwezo wake ni mdogo mno.
 
Kwa taarifa nilizozisikia ni kwamba Mgunda aliweka masharti.

1 apewe mkataba unaotambulika kabisa.

2 kama atakuja kocha Mkuu, yeye asitolewe awe msaidizi na sio kocha aje na msaidizi wake.

3 amekataa dharau, mambo yakiwashinda ndio mnamkumbuka so this time around anataka heshima ifate mkondo wake.
 
Heshima imefuata mkondo wake.
 
Hizo ndo terms nzuri za mkataba, alikuwa anaenda vizuri wakamweka kando,leo wakifeli wanamkimbilia tena ,ni madharau kuonekana upo cheap
 
Hawa takukuru inawahusu
 
Hata Mimi nilishangaa kumuona matola Tena.
 
KAMA NI HIVYO BASI KACHEZA KAMA PELE.
 
Naona sasa tunamtaka ANDAZI!
 
huyo ni mganga wa kienyeji sio kocha
 
Daniel cadena Ni kocha makipa imekuaje kawa kocha mkuu

Simba inatangatanga mno
 
Acheni ramli za kipuuzi. Anafungwa Guardiola simbuse Mgunda? Tatizo la vijana wengi wa bongo wameanza kushabikia mpira juzi. Unataka Simba washinde kila mechi, league ya nini sasa.
 
Mbona bado kabisa Simba anaacha point kwa Azam na kipigo heavy acha kile Cha Yanga walipiga kwa kuonea huruma Azam ni atafuta kabisa magoli ambayo Simba kafunga yani itasoma -muanze upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…