DOKEZO Uongozi wa The Guardian haujatulipa mshahara miezi mitano lakini Raia Wa kigeni wanalipwa kama kawaida

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tafuteni kazi nyingine huku mkiendelea kufuatilia madai yenu😭
 
Makampuni yote ya IPP kwenye suala la mishahara ni kivumbi
 
Pole sana mkuu!
Kama sio mnumuzi wa mandazi unaweza kaa miaka 10 bila kugusa gazeti
 
No offence ila nadhani inatakiwa uwe wa kitofauti sana KUSOMA/ KUNUNUA MAGAZETI siku hizi so possibly lazima biashara iyumbe tuu.
 
Hali ni ngumu ndio maana mtu ukipata upenyo bora ukimbilie kwenye taasisi zinazojielewa au serikalini

Nina imani, ni bora mara alfu uimbe mapambio lakini mpunga unasoma kuliko kujikuta mwanaharakati uchwara ilhali unatembeza bakuli

All in all, fuatilieni haki zenu kupitia vyama vya wafanyakazi natumai mtapata msaada mna kila sabau ya kulipwa kwa sababu mnafanya kazi na mna-deliver
 
Hiyo biashara ya magazeti haifai wengi tunapata habari tena za muda huo huo kabla kuandika ktk magazeti yenu. Sikumbuki lini nilinunua gazeti. Ujue watumia simu line mill 70. Kama milioni 20 wana simu janja ambao ndio wana uwezo wa kunua gazeti na wengi hawanunui wanaopata news toka kwenye simu sioni biashara nzuri ya magazeti. Ujue watu wavivu kusoma magazeti na vitabu.
 
Loh poleni sana sana
Nimewahi kufanyakazi hapo The Guardian, nilipitia haya mazonge na kuachana kazi baada ya kulipwa.

The Guardian inaendeshwa kisela sela na ina ubaguzi fulani mbaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…