Uongozi wa timu ya Prisons utafute kocha mwengine

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Jana, Tanzania Prisons ilicheza na Somba katika mechi ya ligi (bahati nzuri huku nilipo umeme ulichukuliwa) na matokeo ilifungwa 3-1.

Leo katika kufuatilia toka kwa wachambuzi wetu(!!!) nimesikia kocha wake wakati wa mahojiano baada ya mechi akilalamika kuwa wachezaji wake hawamuelewi anapowaelekeza.

Hili ni tatizo kubwa na ni kukiri kushindwa kuiongoza timu ni ushauri wangu kwa uongozi wa timu hiyo kumtafuta kocha mwengine mapema kabla jahazi halijazama lote.
 
Ungejiridhisha zaidi kwa kuangalia marudio ya mchezo huo ili ulinganishe uchezaji wa timu na hoja ya mwalimu.
 
Minziro alikuwa sawa
Kazi ya kocha ni kuwapa mbinu wachezaji then wao wazitumie uwanjani.

Sasa wakifika uwanjani wanafanya ujinga
Kumbuka ni wa mwisho hao
 
Minziro ni mjinga,akicheza na simba anakamia game sana tofauti akicheza against yanga,ukiikamia simba utafungwa tu
 
Ndo ukaseme hadharani Wachezaji wangu hawafundishiki? Kwa kauli hiyo Mkuu, Minziro hafai.
Sahihi mkuu. Yeye ni kocha na kwa kutoa kauli hiyo moja kwa moja kwenye vyombo vya habari inawaathiri wachezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…