Mtoa mada, nadhani tafiti kwanza utendaji kazi wa hizi gari. Nafahamu kidogo kuwa baadhi ya gari ni semi na express....ikitoka kimara kwenda kivukoni..kama ni asbh ikishashusha abiria kivukoni inageuka kurudi kimara bila kupakia kituo chochote hadi kimara...wakati zipo zingine zitapitia kila kituo...kuna wakati kadri ya muda, inaweza ikashusha na kurudi yard bila abiria,,,,jamani mfumo wa hizi si kama daladala, kwamba lazima ijaze ndo iondoke, kwakuwa zinapishana kwa muda fulani, basi kila dereva kapingiwa namna ya kufanya na wamewekewa tracking system gari zote, pale jangwani wanazimonita; hivyo kuna wakati wanaziamuru baadhi ya gari zilirudi yard, wakati mwingine kuziongeza barabarani nk....pia kila kituo kimefungwa camera system inayoonekana kule jangwani...hivyo hata yale malalamishi ya kuwa tunajaa sana vituoni bila gari kuja wanazidi kutatua mdogo mdogo...changamoto niliwahi sikia kuwa ni kwenye makutano ya barabara hasa ubungo na magomeni wakati Askari wanapoongoza kuliko Taa zinapo ongoza; ndio maana kuna wakati gari zinajazana mataa...hivyo kuaharibu ile interval ya hizi gari vituoni....
Kwao wao si hasara kutembeza gari bila abiria hasa kama wameamulu lirudi yard au liende haraka kituo fulani cha mwisho...ingekuwa daladala si mpaka wajae..sababu hesabu ni kwenda na kurudi....hawa kazi yao ni kubeba abiria ambao wameshalipia tayari...sio wanaongoja kulipia..ndio maana hakuna nauli ya kubargain, wala kumngoja mtu kituoni...