Uongozi wa veta wafuta trade test kinyemela kinyume cha sheria

Nitasemakweli Daima

New Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imefuta mitihani ya Trade Test kinyemela kinyume cha Sheria ya Bunge Na. 1 ya 1994 iliyounda Mamlaka hiyo. Mfumo wa Trade Test unatambuliwa kisheria kwa mujibu wa vifungu 6(2)(g)(ii) na13(2)(d) vya sheria hiyo.

Uongozi wa VETA ulifanya maamuzi ya kuachana na Trade Test na badala yake mfumo mpya wa Competence Based Assessment (CBA) umeanzishwa. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na VETA, mwisho wa mitihani ya Trade Test Grade III ulikuwa Mei 2012, Trade Test Grade II ni Mei 2013 na Trade Test Grade I ni Mei 2014.

Mabadiliko haya yamepata baraka za Bodi ya Elimu na Mafunzo Ya Ufundi Stadi (VET Board) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Hapa Bodi pamoja na Waziri wameingizwa mkenge kwa kuwa wameridhia chombo cha umma kuvunja sheria iliyowekwa na Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Swala la Trade Test lipo katika sheria mama ambayo licha ya kufanyiwa marekebisho mwaka 2006, Trade Test haikuondolewa wala kubadilishwa. Chombo pekee chenye mamlaka ya kubadilisha kifungu cha sheria ni Bunge. Uongozi wa VETA umepata wapi ubavu wa kubadilisha kifungu cha sheria ya nchi? Hata Waziri anayesimamia utekelezaji wa sheria hiyo halioni hili?

Licha ya uvunjifu wa sheria, viongozi hao pia wamejaa ubabaishaji. Wanalazimisha vyuo vyote vifuate mfumo huu wa CBA ambao bado haujatengamaa. Wanafunzi wengi kufeli katika mtihani wa Desemba 2012 ni ushahidi tosha. Wanafunzi wanaojiunga vyuo hivi ni darasa la saba na kidato cha nne failures. Hawa unawaambia wasome Technical Drawing, Engineering Science, Mathematics, English, Preventive Maintenance, n.k. Hiki ni kichekesho. Unatarajia darasa la saba na Form Four failures wakafanya vizuri katika masomo hayo? Eti wanasema wanataka wakimaliza VETA waendelee na masomo hadi chuo kikuu! Wamesahau kuwa sheria inasema watoe mafunzo yatakayowawezesha vijana kuajiriwa au kujiajiri na sio kuendelea na masomo ya juu. Huu ni upotoshaji mkubwa.

Halafu jamani inakuwaje wanavunja sheria ilhali wanae mwanasheria wa Mamlaka. Anafanya nini huyu. Jamani mabilioni mengi yanapelekwa VETA kila mwaka. Tunataka tuone value for money na sio madudu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…