Uongozi wa Yanga acheni kuhujumu timu ili fisadi aonekane wa maana!

Sisi wengine siyo "Great thinkers" kwa ivo tutajie huyo fisadi. Halafu hujaliona Jukwaa la "great thinkers" wenzako ambako ungeiweka hii mada?
Hili ni jukwaa la Great thinkers kama wewe sio great thinker kaa pembeni
 

Utakuwa umetumwa na mzee akilimali wewe si bure.

Huyo unayetaka kuwaaminisha wana yanga kuwa ni fisadi si alipelekwa mahakamani na akashinda na kesi nyingine DPP akabwaga manyanga?

Sasa wewe unataka kuleta mambo ya maji taka kwenye ukweli? klabu zetu zinataka watu wenye maono au wenye pesa watakaozimwaga bila uchungu kama huyo unayetaka tuamini kuwa ni fisadi.

By the way wenye tuhuma za ufisadi wapo mahakamani kwa sasa kama kina Rugemalira ,Malinzi nw.
 
sisi wanayanga wakongwe hatumtaki fisadi
 
Nsfikiri hii ungeipeleka jukwaa la Michezo sio humu
 
Wewe mpuuzi kweli.

Hao mnaowaita mafisadi wamekuwa wanachama wa ccm miaka nenda miaka rudi. Leo chuki za mtu mmoja ndio zinasababisha mnawita watu mafisadi.

Acheni chuki na visasi maisha ni mafupi sana.
 
Jingalao, Yanga na Simba ni club masikini. Hao wanaoitwa mafisadi miaka yoote ndio wafadhili wa hizo timu kifupi ni team za wahindi na waarabu, Leo hii Simba yuko Mo na Yanga Manji ndio vile tena.. Msimu ujao Mo akiyumba Simba nayo inayumba hayo ndio maisha ya hizi timu.. Leo hii Simba kuna Mo na wenye nchi kila kitu kinaonekana kiko sawa..

Club za mpira ni taasisi na kuziendesha kunahitaji mipango madhubuti na sio hizi blah blah za wanachama na matajiri wanaotafuta umaarufa na njia ya kufanya biashara zao, Maendeleo ya soka huchochewa pia na uchumi wa wananchi wa sehemu husika. Uchumi mzuri kwa watu huvutia mzunguko mzuri kwenye burudani na hivyo ufuatiliaji huu huleta muinuko wa kiuchumi kwenye taasisi za michezo..
 
Hakuna MTU anayewatisha Simba kama Manji..alisema Simba haitachukuwa ubingwa nikiwa mwenyekiti Yanga ikawa kweli...lazima wamchafue lakini 10 June anapewa kiti chake kama kawa..safari hii pre season Mallorca
 
Hakuna hujuma yoyote pale Yanga.

Tukubali hakuna pesa. Yanayoikuta Yanga kwa sasa, yataituka Simba Mo akiondoka. Ni suala la muda naye ataondoka kwa maana Simba imekuwa ni bidhaa, ataiuza muda wowote arejeshe fedha zake na faida juu. Huo utakuwa mwisho wa wapiga kelele wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…