Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Kimsingi kuna makosa yametokea katika kumtimua Gamondi na kum replace mtu ambaye hana uzoefu wa mashindano ya CAF muda mfupi kuelekea kuanza kwa mashindano.
Mechi ya juzi ya Yanga dhidi ya Al Hilal wapo waliona kuwa pengine angekuwa Gamondi mechi ingekuwa nyepesi lakini sidhani kama ingekuwa nyepesi kihivyo kama watu wanavyofikiria.
Yanga imepata tabu kumaliza mechi dhidi ya Kagera, Ken Gold, KMC, n.k isingekuwa rahisi kuifunga timu yenye professional wengi na kocha mwenye uzoefu Ibenge kirahisi hata kidogo. Tatizo la Yanga msimu huu upo katika kubadilisha nafasi kuwa magoli. Gamondi na Saed wote wanakutana na hali hiyo hiyo. Mechi dhidi ya Al Hilal, Yanga ndio wameongoza kupoteza clear chance kuliko Al Hilal na ndio waliyoongoza katika kutengeneza nafasi nyingi za magoli kuliko Al Hilal. Azizi Ki kawa butu, Dube ndio kabisa,
Sina lawama na huyu kocha mpya kwasababu kuna kitu positive nimekiona kutoka kwake lakini lazima itachukua muda katika hili na mashabiki tunataka mafanikio ya haraka kwa kutetea makombe na kutinga robo fainali ya CAFCL.
Kwasasa kuna mambo kadhaa ya kufanya ili kurudisha mambo kuwa sawa.
1) Daktari wa saikolojia anatakiwa kufanya kazi kubwa sana kuwarudisha wachezaji katika hali ya kawaida. Wachezaji wengi wamevurugika kiakili na kutoka mchezoni. Diarra ni mmoja wapo na wengine wengi tu.
2) kuna umuhimu wa kuondoa mipasuko iliyopo ndani ya timu au ndani ya uongozi. Jengeni umoja na ushirikiano ndio jambo kubwa
3) kocha bado hajawajua wachezaji vizuri hivyo kuna umuhimu wa meneja wa timu na mkurugenzi wa benchi la ufundi wasaidiane nae katika kipindi hiki ambacho unatakiwa kushinda mechi upate point 3.
Kwenye ligi bado nafasi ipo kwavile kama kiporo Yanga ikishinda itakuwa ni tofauti ya point 3 tu dhidi ya anayeongoza ligi. Kwenye klabu bingwa pia matokeo ya Tp Mazembe na MC Alger yameipa unafuu Yanga hivyo inabidi iende kupambania point 3 ugenini kitu ambayo kinawezekana ukizingatia kuna mechi nyingi tu Yanga kashinda akiwa away. Kazi kubwa kurudisha umoja, ushirikiano na mentality ya wachezaji ikae sawa pia na fitness ya wachezaji.