Uongozi wa Yanga makosa ya msimu uliopita tusirudie tena

changaule

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2020
Posts
6,039
Reaction score
10,151
Awali napongeza uongozi kwa kuweza kukamilisha usajili wa wachezaji, japo sijajua kama usajili umekamilika au bado kuna wachezaji wengine watakaosajiliwa.

Kwa uzoefu wa mpira ni kwamba usajili unaweza kulipa au usilipe ni sawa na kamari kuna kufanikiwa na kutofanikiwa hivyo sio jambo la kutamba au kuwa mnyonge kwa kusikia tu majina ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu hadi pale msimu utakapoanza na tukashuhudia watakachotupa.

Niende kwenye swala la msingi;. Msimu uliopita viongozi mlitukosea sana kwa kutokuwa na malengo na mikakati ya timu kufanya vizuri klabu bingwa jambo ambalo limetufanya tusifike mbali.

Tulifanya makosa kadhaa ikiwemo ufinyu wa maandalizi ya timu (kutopata muda wa kuandaa timu na pia kutopata michezo ya kirafiki ya kimataifa walau tatu za kujipima nguvu) kutokamilisha kwa wasaa ITC za wachezaji wapya waliosajiliwa.

Hivyo naushauri uongozi kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa watafutiwe ITC zao mapema ili waitumikie timu katika michuano ya klabu bingwa hatua ya awali. Pili ni kuhakikisha timu inaandaliwa mapema na pia kupata mechi kadhaa za kuwafanya wawe na match fitness.
 
ushauri mzuri sana wa kufanyiwa kazi
 
Halafu waache zile mambo za kupeleka timu kwenye maeneo yenye baridi kali, mfano kule Morocco! as if wanaenda kucheza mashindano kwenye nchi zenye baridi kali, kumbe yalikuwa ni maamuzi tu ya kukurupuka.
 
Kambi ipigwe bongo (Avic town), tupate mechi 3:za kujipima nguvu kutoka S A, Sudan na Uganda (Kaizer au Orlando, Elmerek au Alhilal, na Vipers) tukihitJi ya nne twende Zambia tucheze na Zanaco au Zesco au tuwaombe Petro de Luanda ya Angola. Tukiweza tutakuwa vizuri.
 
Sawa sawia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…