Uongozi wa Yanga sc unaendelea kukomaa na Fistoni kalala Mayele.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Makamu wa Rais wa klabu ya Young Africans Arafat Haji, amewaondoa wasiwasi Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kuhusu mustakabali wa Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele, ambaye anadaiwa kuwindwa na baadhi ya Klabu za BArani Afrika.

Kufanya vizuri kwa Mayele akiwa na Young Africans kwenye Michuano ya Kimataifa kumezitamanisha klabu kadhaa kuhitaji huduma ya Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa Wananchi.

Baadhi ya klabu zinazotajwa kuwania saini ya Mshambuliaji huyo kinara wa mabao katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu akifunga saba ni Kaizer Chiefs, Orlando Pirates za Afrika Kusini, US Berkane na Raja Casablanca za Morocco.
 
🟩🟨
 
Nikiwa Mipang'ang'a toka kambini umbumbumbuni nabariki huyo Mayele aondoke tu, tuna Kibu Denga Mzee wa mashuti ya mbali atatupatia CAFCL, NBC PL na makombe mengine tele.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…