Uongozi wa Yanga ukikejeli, Wanaume tunapambana kuingiza timu nne

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
NAJUA WAJUA ILA NATAKA KUKUJUZA ZAIDI NA ZAIDI KUHUSU CAF INTERCLUB.

Na: Hashim Mbaga. 14/03/2022

USHIRIKI WA TIMU ZA TANZANIA KUPATA UWAKILISHI WA TIMU NNE MISIMU IJAYO.

Tanzania katika Msimu huu wa 2021/2022 kwenye CAF INTERCLUB inawakilishwa na Simba Sports Club ambayo ipo kwenye hatua ya Makundi (Group Stage) ya CAF Confederation Cup baada ya Timu zingine Yanga, Azam na Biashara United kutolewa katika hatua mbalimbali zilizopita.

MSIMU UJAYO WA 2022/2023 CAF INTERCLUB.

Kwa mujibu wa Takwimu za nchi kuwania nafasi 12 za juu ambazo ndio zinaipa nchi Ushiriki wa Timu nne katika Mashindano Mawili Tofauti mpaka sasa Tanzania ipo ndani ya nchi 12 na kati ya hizo nafasi 3 zipo katika Kinyanganyiro kikali sana kwa kuhusisha jumla ya nchi 6 toka ndani ya nchi 12 za juu (Ushiriki Timu 4) zipo nchi 3 za Tanzania, Nigeria na Zambia wakati 3 zingine zipo Nchi za Cameroon, Libya na Ivory Coast zilizokuwa na ushiriki wa kawaida (Ushiriki Timu 2).
Katika Nchi Hizo 6 ni nchi 5 tu (Kasoro Nigeria) ndio zinazoshiriki mashindano zenye jumla ya Timu 6 na zote zipo Caf Confederation Cup 2021/2022.

TWENDE KWENYE TAKWIMU

TANZANIA
Msimu ujayo wa 2022/2023 Tanzania inakuwa na Mwanzo wa POINT 20.5 kabla ya kuongezwa Point za Simba itazopata msimu huu sasahivi mashindano yanavyoendelea.
1. Simba ikiwa ya Nne kwenye Kundi Tanzania itabaki na Point 23
2. Simba ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Tanzania itabaki na Point 25.5
3. Simba ikivuka kwenda Robo Fainali Tanzania itakuwa na Point 30.5

NIGERIA
Msimu ujayo inaanza na Point 26 na hakunanyongeza ya Point msimu huu kwakuwa Nigeria haina Ushiriki wa Timu katika Makundi.

ZAMBIA
Msimu ujayo inaanza na Point 22 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu kwa Ushiriki wa Timu ya Zanaco iliyopo Makundi
1. Zanaco ikiwa ya Nne kwenye Kundi Zambia itabaki na Point 24.5
2. Zanaco ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Zambia itabaki na Point 27
Kutokana na Matokeo ya sasa havuki zaidi ya hapo.

LIBYA
Inawakilishwa na Timu 2 zote Confederation Cup (Al Alhy Tripoli na Al Ittihad)
Msimu ujayo inaanza na Point 8 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu wa Timu zake zilizoingia Makundi.
1. Timu zote mbili zikitolewa katika makundi Libya itabaki na Point 13
2. Timu moja ikiingia Robo Fainali na Moja ikashindwa Libya itakuwa na Point 23
3. Timu zote mbili zikiingia Robo Fainali Libya itakuwa na Point 28
4. Timu moja zaidi ikicheza Nusu Fainal Libya itakuwa na Point 33

CAMEROON
Msimu ujayo inaanza na Point 12 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu kwa Ushiriki wa Timu ya Coton Sports iliyopo Makundi
1. Coton ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Cameroon itabaki na Point 17
2. Coton ikivuka kwenda Robo Fainali Cameroon itakuwa na Point 22
3. Coton ikivuka Nusu Fainal Cameroon itakuwa na Point 27
4. Coton ikicheza Fainal Cameroon itakuwa na Point 32

IVORY COAST
Msimu ujayo inaanza na Point 5.5 kabla ya kuweka nyongeza ya msimu huu kwa Ushiriki wa Timu ya Asec Mimosa iliyopo Makundi
1. Asec ikiwa ya Nne kwenye Kundi Ivory Coast itabaki na Point 8
2. Asec ikiwa ya Tatu kwenye Kundi Ivory Coast itabaki na Point 10.5
3. Asec ikivuka kwenda Robo Fainali Ivory Coast itakuwa na Point 15.5
4. Asec ikivuka Nusu Fainal Ivory Coast itakuwa na Point 25.5
5. Asec ikichukua kombe Ivory Coast itakuwa na Point 30.5

HITIMISHO

Katika kujihakikishia nafasi Tanzania ni Lazima @simbasctanzania kuingia ROBO FAINALI kuwa na Point 30.5 ndio itafanya kuwa na 95% wakati Tukisubiria Kila hatua Wapinzani wanavyopungua na kwisha kabisa kwa ufafanuzi huu:

1. Tanzania Timu moja (Simba) na Libya Timu zake Mbili (Al Ittihad na Al Alhy Tripoli zote zikiingia Robo Fainali ina 95% ya kupata nafasi mojawapo bila kuangalia matokeo yeyote maana watakuwa wamechukua nafasi za Zambia na Nigeria.

2. Asec Mimosa ya Ivory Coast na Coton Sports ya Cameroon ili kupata nafasi lazima waweze kupita Nusu Fainal ndio hesabu zinaweza kueleweka vizuri kidogo.

3. Simba isipoweza kuingia Robo Fainali ila ikawa nafasi ya Tatu katika Kundi lake Tanzania itatakiwa kupata nafasi ni lazima Zanaco kwa maana ya Zambia ishike nafasi ya nne katika kundi lake maana inagombania nafasi 3 au kubaki ya 4 tu kwa sasa wakati huohuo Timu za Cotton Sports ya Cameroon na Asec Mimosa ya Ivory zisiweze kuendelea mpaka kufika Nusu Fainal hapo ndio Nafasi ya Uwakilishi Timu nne itaweza kubaki Tanzania.

IELEWEKE WAZI Kutokana na ushiriki wa Simba na kuongeza Point inaweza kufanya Tanzania ikawa moja ya nchi zitakazotoa Timu nyingi msimu ujayo katika Mashindano ya CAF kulingana na Taratibu zitakazotolewa na CAF katika ushiriki wa Timu kwenye Champions League, Confederation Cup na African Super Cup.
 
Yote hayo bado Simba Sc inaonekana haina lolote kwa baadhi ya wajinga waliojaa hapa Tanzania.

Kuna miaka fulani nyuma team fulani ilifululiza kuchukua ubingwa na ikafanikiwa kuingia kwenye hayo mashindano lakini tuliambulia aibu na kuonekana viande, na hakuna hata msimu waliosaidia kuingiza team nne, wao walijali kupanda ndege pekeao kwa kujiita "wakimataifa" bila kufanya lolote huko.

Simba Sc kapata nafasi mara ya kwanza tu akafika hadi robo, hizo points kwa 70% ni jasho la Simba Sc.
 
Ngoja waje wale jamaa wenye roho za husuda . Utokoma![emoji2][emoji1][emoji2]
 
Kumbe lile jina la kimataifa walilipata kwasababu ya kupanda ndege na hawasemi
 
Kumbe lile jina la kimataifa walilipata kwasababu ya kupanda ndege na hawasemi
Kipindi kile wanaenda kwenye mashindano nje, Jerry Muro akawajaza kwakuwaita wakimataifa na kuiita simba ya Matopeni. Ilikuwa ni kwasababu ya zile ndege walizokuwa wanapanda kwenda kutalii.
 
Ungeanza kwa kueleza vizuri Simba walikuwa club wakatolewa, tena wakiwa nyumbani ndio wakaangukia huku viti maalum.
 
Hawa Wachambuzi hawamuoni Kabisa BM3.....!
Kuna Chuma Kimoja Alikipiga Kikagonga posti Fantastic... !

Wachambuzi Wameng'ang'ania Refa kawanyima goli Sio Off side....!

Next Match aje Kuchezesha Mr Kilo Mia nane...! Msukule awe Line 1 ...! na CAF Wamlete line 2 baaasi.
 

Umeandika kwa uchungu kabisa mzee baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…