Asalam wakuu,
kijana wangu ana umri wa miezi kumi na wiki mbili.
kidume huyu kaanza kuota meno (hayaonekani kwa macho) ya juu tofauti na ilivyo kawaida kuanza ya chini.
PILI meno yanachelelwa sana kuota maana hadi sasa hayaonekani bali hadi uguse fizi ya juu mbele ndipo utahisi mushrooming of meno je kwa umri huu aliokuwa nao ni kawaida au ana matatizo?
Je, watoto wa namna hii wanakuwa na tabia zipi?
Je, kuna uhusiano wa kuwahi au kuchelewa kwa meno na uongeaji wa mtu (kuongea sana na kinyume chake)?
Mwenye uzoefu ashushe mambo hapa najuwa humu kuna wazazi kibao na wataalam pia?