SoC04 Uozo mifumo ya maombi ya ajira za serikali

SoC04 Uozo mifumo ya maombi ya ajira za serikali

Tanzania Tuitakayo competition threads

Even MOre

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
204
Reaction score
298
Nimekuwa nikifatilia muda mrefu sana toka Serikali imebadili baadhi ya maombi ya ajira kuwa yanaombwa kwa njia ya mtandao (Online Application) nina kama miaka 4 sasa nafanya kazi hii ya kusaidia watu kutuma maombi kwa njia ya mtandao (Internet services) pia huduma ya mifumo ya Kiserikali.

Hoja iko hivi kwa hii miaka kadhaa kumekuwa na shida kubwa pale tu ambapo Taasisi flani ya Serikali ikitangaza nafasi za kazi ziwe za muda au za kudumu basi kutatokea shida ya mfumo husika wa maombi ya kazi kushindwa kufanya kazi hadi zitakapobaki siku kadhaa kufikia mwisho wa maombi (Deadline) kama siku 1&2 ndipo mfumo hurejea na kuweza kufunguka kwa urahisi kabisa.

Nimeshuhudia haya mfano kipindi cha maombi ya kazi za Ualimu, Kada ya Afya, Maombi ya Sensa, nk mpaka maombi yanayoendelea ya kujiunga na Jeshi la Polisi ambayo deadline ni kesho, toka watangaze mpaka leo mfumo haufunguki licha ya shida internet nchini lakini mifumo mingine ya Serikali inafunguka na kutumika bila shida kabisa.

Maswali yangu ni haya:-
1. Ikiwa kuna shida ya mfumo kuwa na watumiaji wengi (Traffic jam) kwanini mifumo haiboreshwi kwa miaka yote hii ambapo wanajua kila wakati wanapotoa matangazo watu waombe kwa njia ya mfumo wanaona mfumo unalemewa na watumiaji?

Kama ni mfumo kuzidiwa na watumiaji, kwanini wasiongeze Servers zenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kuendana na muda wa maombi uliopangwa?

2. Ikiwa hakuna wataamu waajiliwa wa Serikali wanaoweza kutatua changamoto hii ambayo imekuwa inajirudia mara zote, kwanini Serikali wasiingie ubia na makampuni ya Teknolojia yenye Wataalamu wabobezi (Ukweli Serikalini hakuna wataalamu walio bora wengi kanjanja).

3. Ikiwa kunakuwa na shida ya mfumo inakuwaje baadhi ya watu wanaweza kufanya maombi? (Hapa inaingia dhana kuwa kuna namna inafanyika)

4. Ikiwa tunataka kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia Dunia lakini hatutaki kuboresha mifumo yetu na kutaweka watu wenye ujuzi na waliobobea bila kujali Elimu zao, kwanini tusibaki kwenye utaratibu wa zamani wa maombi kutumwa kwa njia ya mkono?

Nawasilisha
 
Upvote 2
Kama ni mfumo kuzidiwa na watumiaji, kwanini wasiongeze Servers zenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kuendana na muda wa maombi uliopangwa?
Tuna changamoto ya nia madhubuti tu hapa bro.

Ikiwa tunataka kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia Dunia lakini hatutaki kuboresha mifumo yetu na kutaweka watu wenye ujuzi na waliobobea bila kujali Elimu zao, kwanini tusibaki kwenye utaratibu wa zamani wa maombi kutumwa kwa njia ya mkono?
Kwa kweli pamoja na changamoto zote, asee ziboreshwe tu hizihizi njia za online. Zimesaidia sana kuweka urahisi wa kuomba kazi kuliko kurudi tena zama za mawe. Changamoto zifanyiwe kazi tu
 
Tuna changamoto ya nia madhubuti tu hapa bro.


Kwa kweli pamoja na changamoto zote, asee ziboreshwe tu hizihizi njia za online. Zimesaidia sana kuweka urahisi wa kuomba kazi kuliko kurudi tena zama za mawe. Changamoto zifanyiwe kazi tu
Kaka shida ni kwamba tunataka kuingia katika matukizi ya teknolojia ambayo bado hatukuweka maandalizi yake vema na miaka mingi mifumo ya Serikali inalalamikiwa lakini hawafanyi maboresho.
 
Jamani tafadhali unapopita hapa bonyeza neno VOTE tuweze kusonga mbele 😁😁
 
Back
Top Bottom