The Fixer
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 1,365
- 594
Wadau,
Heshima kwenu ! Kwa muda wa siku chache nlizokaa kwa ajili ya kupata huduma ya forodha katika mpaka huu wa Horohoro baina ya Kenya na Tanzania kwa upande wa Tanga nimegundua madudu mengi sana juu ya usalama wa Tanzania kama Taifa !
Mpakani Horohoro kuna ombwe kuu la usalama kwani mizigo mbalimbali na abiria hawakaguliwa ipasavyo kukidhi haja ya dhana nzima ya usalama kwa mapana yake
Kwa mfano, Tanzania kama soko kuu la madawa ya kulevya lango kuu limekuwa ni Zanzibar, Bandari ya Tanga na hasa lango la Mombasa kwa kutumia mpaka huu. Katika dodosa mbalimbali nilizofanikiwa kuzifanya hakuna mbwa kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita na siku chache zilizopita wamemleta mbwa ambaye hata hivyo hawamtumii kikazi zaidi ya kumfunga tu kwenye nguzo ya banda la polisi, mbwa huyo hata akibweka namna gani ? Pindi bus ama gari loloote likipita hafunguliwi ili kuweza kutambua nini anachobwekea
Swala lingine lililonishanganza ni ukaguzi wa mizigo unavyofanywa " kiushkaji " badala ya kuwa ni professional duty. Kwa mfano mzigo wa nazi, maembe ama mazao mengine yanayomwaga tu kwenye bodi la gari hakuna mahala pa kuyamwaga kwanza na kuyarudishia ili kujiridhisha bila ya shaka yoyoote juu ya uingizaji wa bidhaa mbalimbali zenye madhara kiuchumi na kijamii hasa madawa ya kulevya kwani nani anayejua kuwa pale mwanzo wa bodi ya gari chini kabisa kumeweka gunia la nini ?
Mtu mwingine aliyeununua mpaka huu ni Willy Enterprises. Huyu anafanya biashara ya usafirishaji wa udongo wenye madini anuwai kwenye nchini Kenya. Ukaguzi wa shehena zake haukaguliwa vya kutosha na wana usalama wetu na maafisa wa forodha kwani zipo habari kwamba katika baadhi ya shehena zake za udongo pia huweka sukari, bangi na bidhaa nyingine nyingi ambazo hazilipiwi ushuhuru wowote na ni makosa legally kuyauza nje ya nchi.
Hata baada ya Bunge kupitia kwa waziri mkuu kupiga maraufuku Tajiri Willy kuusafirisha udongo huo kutoka milima ya pare lakini tajiri huyo bado anaendelea na Mbunge wa eneo husika amekaa kimya bila harakati zozoote za kuzuia jambo hilo
Ukiacha wenzetu wakenya ambao mpaka wao ulikuwa na uzio wa walau mita mia 3 ( 300 mts ) kabla ya ujenzi mpya wa kuuzungushia mpaka woote uzio ukidhaminiwa na World Bank na walau kudhibiti uingiaji holelaa wa watu wa ukanda huu , Sisi hatukuwa na uzio wowoote na kufanya uingiaji holelaa wa watu bila ya vibali vyovyoote
Kwa ufupi tu mpaka huu ndio umekuwa lango kuu la uozo woote unaopatikana Tanzania kupitia na wakuu wa idara zote za usalama na forodha wapo na maisha yanaendelea tu kama kawaida.
The fixer,
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums