Jamani TTCL broadband mnatufilisi wateja wenu. Sisi ni wateja wenu wa miaka mingi sana. Sasa hii tabia mlioianzisha hivi karibuni sio nzuri kabisa. Tukiweka pesa kwa ajili ya internet ya Broadband baada ya wiki 2 mnafunga hata kama kuna hela imebaki. Halafu tukiwafuata mnasema tulipie shilingi elfu 25,000/- hivi mnafikiri pesa zinaokotwa? Mwezi uliopita nimelipia sh. 25,000/- mwezi huu mmenikatia tena mnaniambia nilipie tena sh. 25,000/- bado sijaweka hiyo vocha ya sh 10,000/-. Huo ni wizi wa kimachomacho. Mimi ni mwananchi wa kawaida wa kipato cha chini nimebahatika kuwa na line na simu nikabahatika kuwa na computer yangu ya Pentium lll na nikaamua kuweka na internet sasa kwa mtaji huo mnaotupeleka wa kulipa pesa nyingi hatutaweza. Tulitegea TTCL ni ya serikali ipo kwa manufaa ya wananchi wote kumbe tumekosea inawalenga wenye nazo. Tunaomba mjirekebishe. Mnatuumiza kwa mwendo huo.