Uozo Vodacom na TCRA

Uozo Vodacom na TCRA

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Morning wakuu!Naomba niende kwenye mada yangu moja kwa moja.

Siku ya jumatatu tarehe 30/11/2020 niliishiwa muda wa maongezi na nikaamua kujiunga kifurushi cha TSH 2,500/ ambapo nilipewa dk50 kwenda mitandao mwingne na dk180 voda kwenye voda tu.

Maana yake nilikuwa na jumla ya dk230,cha kushangaza imefika tarehe 3/12/2020 napiga simu naambiwa sina salio (nilijiunga kifurushi cha wiki).Mara nyingi nikiongea sana kwenye simu natumia dk5 tu tena mara mojamoja.Nimeenda vodashop wanajikanyaga tu,Nafuta wakili mbobezi niishitaki hii kampuni kwa kuniibia mchana kweupe naomba kama kuna wakili anaweza kuhandle hii kesi aniPM (nina ushihidi wote).
Najiuliza sana maswali yafuatayo;

TCRA hawaoni huu wizi?maana naamini wanaibia wengi.
TAKUKURU hawaoni huu wizi?
VODACOM wana tofauti gani na wahujumu uchumi?
 
Ungekwenda kushtaki kwanza kabla ya kuja kutupasha hapa!
 
Uliunga kifurushi tare..30-12-2020 hadi tare..3-1-2020 "basi sawa"
 
Ungefuatilia kwanza kujiridhisha kama kweli hujatumia hizo dakika....kaombe wakupe taarifa fupi ya simu yako ukague. Maana unaweza ukajipanga hatimaye ukajikuta wewe ndio umejikanganya.
 
Hii inchi ina vituko sana...kifurushi cha 2500 tu unalalamika, ada za mawakili ndo utaziweza?
Anyway uliwezaje kujiunga na kifurushi tarehe 30/12/2020 while ndo kwanza tupo tarehe 5/12/2020?
 
nina wasiwasi na uelewa wa mwandishi kama anashindwa kuanfika tarehe inawezekana pia alijiunga kifurushi cha Sikh akidhani cha week
 
Back
Top Bottom