Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kuna aina nyingi za mapambo yanayotumika katika kupendezesha nyumba zetu. Aina mojawapo ni maua halisi (natural flowers) ambayo huleta muonekano mzuri, uhai na harufu ya kuvutia.
Ili kuweza kupata thamani halisi ya maua yako ni vyema ukatumia chombo (vessel) kizuri cha kuvutia na ukayaweka kwa ustadi ili yaweze kudhihirisha uzuri wake wa asili.
Kabla ya kuanza kupanga maua yako kwenye chombo husika, kwanza hakikisha chombo hocho ni kisafi kabisa bila kuwa na vumbi au uchafu wa aina yoyote. Kisha weka maji kiasi ili maua yako yaweze kuishi kwa muda mrefu zaidi.
Maua yako yakate katika urefu sawa kulingana na aina ya maua. Hapa namaanisha kama ni maua ridi basi yote yawe urefu wa kulingana, hata kama utachanganya maua tofauti katika chombo kimoja hakikisha yale yanayofanana yana urefu sawa.

Ukiwa unataka maua yawe marefu tumia chombo kirefu chembamba (kikiwa cha kioo kitapendeza zaidi) na akama ni maua mafupi basi tumia chombo kifupi na kupana ili kuleta muonekano wa kuvutia.
Vile vile unaweza weka viua vidogo vidogo kwenye vessel ndefu ya kioo na kumiminia maji safi, upambaji huu huvutia sana na huleta muonekano uliotulia ndani ya nyumba. Unafaa sana maliwato na chumba cha kulala.

Maua yana aina nyingi sana za upambaji, hizi ni cheche tu jaribu leo na utaona jinsi ambavyo nyumba yako itakuwa ya kuvutia na kukufanya ujisikie vizuri siku nzima.
womenofchrist blog