Upandikazi wa mche (grafting & budding) kwenye zao la parachichi

Upandikazi wa mche (grafting & budding) kwenye zao la parachichi

s_ng21

New Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
2
Reaction score
5
[emoji271]Grafting na budding ni mbinu za bustani (Horticultural techniques) ambazo zinatumika kuunganisha sehemu za mimea miwili au zaidi ili zikue kama mmea mmoja.

[emoji271] Vyanzo mbalimbali vinaelezea nyanja mbalimbali za utofauti wa mbinu hizi mbili mfana kwenye nyanja za uimara, ubora, matumizi , aina n.k japokiwa mbinu hizi mbili kimsingi hutofautiana kwenye namna ya UNGANISHWAJI WA MMEA/MCHE [emoji271]kama ilivyoelezwa hapo juu.

UTOFAUTI ni kama ifuatavyo
Kwenye grafting sehemu ya juu ya mmea / mche mmoja (KIKONYO) hukua kwenye sehemu ya mzizi ya mmea / mche mwingine yaani, sehemu ya ahina ya mmea mmoja hupachikwa kwenye kwenye mmea mwingine [emoji271]

Hivyo kwenye GRAFTING, kikonyo ni sehemu ya shina.

Kwa upande mwingine ( BUDDING).

Kwenye budding, mche chipukizi kwenye mti mkuu (bud au kikonyo) huchukuliwa kutoka kwenye mmea mmoja na kukuzwa kwenye mmea mwingine. Mti unaotumika kukuzia chipukizi (bud) ya mti mwingine huitwa mmea mzazi[emoji271]

Hivyo kwenye budding, kikonyo ni mche chipukizi / a bud.

VIGEZO VYA KUFANYA GRAFTING BORA
1. Utengamano wa kikonyo na shina mzizi (Compatibility of scion and root stock)

Kwa kuwa grafting inahusisha uunganishwaji wa kikonyo na shina mzizi (joining of vascular tissues), mimea inayokosa mfumo wa mishipa mfano nyas, migomba, vitunguu, mahindi, mtama, mpunga (lacking vascular cambium) n.k haziwezi kufanyiwa grafting. Kwa ujumla kadiri mimea miwili inavyokua na mfanano zaidi wa asili (vinasaba / genes). Uwezekano wake wa muunganiko (grafting) unaongezeka. Grafting has a high success rate when performed with plants of the same family and genera (identical clones and intra-species crops).

2. Mpangilio wa mishipa na mgandamizo wa uunganishwaji (Cambium alignment and pressure)
Mifumo ya mishipa ya shina mzizi na kikonyo lazima iunganishwe kwa kukazwa kisawa sawa kuelekea uelekeo wa ukuaji wa kawaida (normal growth). Mpangilio sahihi na mgandamizo toshelevu inachochea mishipa kuunganikana kwa haraka, hivyo kuruhusu virutubisho na maji kusafiri kwa haraka kutoka kwenye mizizi kwenda kwenye kikonyo.

3.Kukamilika wakati wa hatua inayofaa kwa mmea
Grafting hukamilika wakati ambapo kikonyo na shina mzizi vinauwezo wa kutengeneza tishu komavu hasa za kuponya kidonda (grafting union). Kwa kiwango kikubwa joto huathiri mmeakipindi cha mabadiliko yake. Kama hali ni ya joto sana (temperature greatly affect plant physiology), grafting njiti huweza kutokea (premature grafting may result).

4. Utunzaji sahihi wa eneo la muunganiko
Baada ya grafting zoezi la kulea miche husika ni muhimu ili kurejea katika hali ya afya bora kwa muda. Vifungashio mbalimbali hutumika kulinda kikonyo na shina mzizi visipoteze maji. Pia kulingana na aina ya grafting, kamba hutumika kuupatia uimara zaidi sehemu ya muunganiko. Wakati mwingine ni vyema zaidi kuondoa machipukizi eneo la chini ya muunganiko (removing suckers / pruning) ili yasizuie ukuaji wa kikonyo.

FAIDA ZA KUFANYA GRAFTING
1. Uharakishwaji wa mti kupevuka (precocity)

Grafting inasaidia mche kufikia mzazi yaani utoaji wa maua na matunda pasipo kupitia ya awali ya ukuaji (kipindi kati ya kuchipua kwa mbegu mpaka ukomavu wake kabla ya uzazi). Kwa miti mingi ya matunda, kipindi hiki hudumu kwa miaka 5, 9 mpaka 15. Kufanya grafting kwa vikonyo vilivyokwisha pevuka inasaidia mche / mti kufikia uzazi ndani ya miaka miwili (2).

2. Dwarfing (kwa lugha ya kiswahili ni kibete)
Ni mchakato unahusisha mzao mpya wa mmea uliobadilishiwa sifa zake asilia za jamii yake mfano kuwa mdogo zaidi / dwarf kwa lengo la kuongeza uzalishaji na ubora wa matunda, kupunguza ajali za wavunaji wa matunda.

3. Urekebishaji
Grafting inasaidia kurekebisha hitilafu kwenye shina la mti ambayo ingezuia usambazaji wa virutubisho mfano kubanduka kwa gome la mti kwa wadudu waharibifu kama vile panya. Katika hali hii grafting huweza kurekebisha na kuunganisha tishu zilizopatwa na hitilafu na kuruhusu usambazaji wa virutubisho kuendelea.

4. Uzalishaji kasi wa mmea chotara
Grafting inasaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa mmea chotara. Miche chotara huchukua miaka 10 au zaidi kutoa maua au matunda kwa mizizi yake ila grafting inapunguza muda wa maua na kufupisha kipindi kuelekea uzazi.

5. Ukinzani wa magonjwa na wadudu
Kwenye maeneo ambayo wadudu wa udongo (soil borne disease / pest) wangezuia kumea kwa aina pendwa ya mmea muafaka huwa ni matumizi ya mmea mzizi unaostahimili magonjwa na wadudu kupitia grafting.

6. Kuubadilisha mmea (changing cultivar)
Grafting inasaidia kuubadisha mmea wa zamani kuelea mmea mpya wenye faida zaidi pasipo kuung'oa ule wa awali. Hivyo kuifanya njia hii kuwa ya haraka zaidi kuliko kupanda upya mbegu nyingine au mmea mwingine ambao hujafanyiwa grafting.

7. Uthabiti wa maumbile (Genetic consistency)
Kwenye kilimo biashara, kwenye uthabiti kwa maana ya saizi, rangi na ladha ya matunda hudumishwa kwa kikonyo chenye sifa zinazohitajika, hasa kwa mimea ya matunda yenye asili ya tabia zaidi ya moja mfano parachichi, embe n.k.

IMG_20220609_152929_089.jpg
 
Pamoja sana Mkuu kwa Elimu ya bure
 
Nimekupata vema kabisa nina maswali mawili Hapo mdau

1.Baada ya grafting yale majani ya chini ya sehemu ya maungio endapo yakitolewa, Huoni Kama mfumo wa photosynthesis kwa mmea utathirika kwa kuyaondoa wkt tunasubiri kikonyo kipya kichipue?

2.Tumezoea kuona grafting baina na mche wa kisasa na kienyeji, Vipi nikifanya baina na Miche ya kienyeji peke yake, Je nayo uzaaji wake utaonekana muda mfupi (miaka miwili) au Kuna delay

Naomba nifumbue macho kidogo juu ya haya
 
Nimekupata vema kabisa nina maswali mawili Hapo mdau

1.Baada ya grafting yale majani ya chini ya sehemu ya maungio endapo yakitolewa, Huoni Kama mfumo wa photosynthesis kwa mmea utathirika kwa kuyaondoa wkt tunasubiri kikonyo kipya kichipue?

2.Tumezoea kuona grafting baina na mche wa kisasa na kienyeji, Vipi nikifanya baina na Miche ya kienyeji peke yake, Je nayo uzaaji wake utaonekana muda mfupi (miaka miwili) au Kuna delay

Naomba nifumbue macho kidogo juu ya haya
1. Majani hayatolewi yote bali hupunguzwa na kubaki machache
2. Grafting inafanywa kwa lengo maalumu, mfano kama umeona mmea mmoja wa kienyeji unazaa sana na mmea mwingine hauzai sana ila unahimili ugonjwa flani/ukame unaweza ukafanya grafting ili kuunganisha hizo tabia ambapo utapata mmea unao zaa sana pia unahimili ukame/ugonjwa flani
 
Grafting ni sanaa moja nyeti sana kwenye sekta ya ukulima. Kuna moja hivi ambayo iliniacha mdomo wazi. Kutoka kwa mkulima mmoja, ambaye alikuwa mfungwa gerezani nchini Kenya. Huwa wanafunza 'skills' kama hizo wakiwa ndani, pamoja na vitu kama useremala, masonry, plumbing n.k, n.k.

Jamaa anatengeneza hela kupitia ukulima wa Pomato(potato & tomato). Viazi na nyanya zilizofanyiwa grafting kwa pamoja, nyanya juu viazi chini. Kama hivi;
Cultivation-of-PomatoS-farmers-trend.jpg
Nakala kuhusu mkulima huyo na kazi yake kwenye jarida la The Standard; Ex convict earns living from pomato, the plant that yields both potatoes, tomatoes
 
Aisee Hii mpya kabisa kumbe Dunia Ina mengi hadi nyanya
 
Back
Top Bottom