Upara sababu ya maradhi ya moyo?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Wanaume wanaoanza kuwa na upara huenda wakakabiliwa zaidi na tisho la maradhi ya moyo kuliko wenzao waliojaa nywele vichwani.


Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan.



Utafiti huu uliowahusisha watu 37,000, ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo.

Hata hivyo, watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.

Shirika linalojikita katika maswala ya maradhi ya moyo nchini Uingereza, limesema kuwa wanaume wanapswa kujichunga wasinenepe kupita kiasi kuliko kuchunga nywele zao.

Kuanza kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa wanaume . Wengi kuanza kukuwa na upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia 80 ya wanaume hao, hupoteza nywele wanapokuwa na umri wa miaka 70.


Watafiti katika chuo kikuu cha Tokyo, walidurusu utafiti wa miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya kuwa na upara na maradhi ya moyo.


Walionyesha kuwa nywele ambazo zilianza kutoweka, zina uhusiano na maradhi ya moyo. Hii ilikuwa baada ya kuzingatia maswala kama umri, na historia ya familia.


Daktari, Tomohide Yamada, wa chuo kikuu cha Tokyo alisema kuwa walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la kupata maradhi ya moyo.


"tuliona hili kama jambo muhimu, lakini halina athari kubwa kama mambo mengine yanayosababisha maradhi ya moyo kama vile uvutaji sigara, unene kupita kiasi na mafuta mengi mwilini pamoja na shinikizo la damu.''


Alisema kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata upara wanapaswa kuanza kuzingatia afya njema ili kujikinga kutokana na maradhi ya moyo


Aidha alisema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa wanaume wenye upara wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.

Maradhi ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini Uingereza.
Mmoja kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya moyo.

Husababishwa na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo pale inapoziba.

Mmoja wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti huu unaibua hisia, wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.Upara,sababu ya maradhi ya moyo? - BBC Swahili - Habari
 
Usije kushangaa hawa watafiti wakaja na mpya ya kwamba watu wenye "vibamia" sio rahisi kupata maambukizi ya VVU.
 


Mh. waziri, sasa naona unanitisha kwani upara wangu nimerithi toka kwa wajomba ila baba yangu alikuwa na nywele nyingi sana. Swali, je nina uwezekano wa kupata haya matatizo ya moyo?
 
Mh. waziri, sasa naona unanitisha kwani upara wangu nimerithi toka kwa wajomba ila baba yangu alikuwa na nywele nyingi sana. Swali, je nina uwezekano wa kupata haya matatizo ya moyo?
Usiogope Rais Mtarajiwa wangu Mkereketwa_Huyu kunywa sana maji ya Uvuguvugu na kitunguu saumu hutopatwa na Maradhi ya Moyo.Chanzo https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/365977-muujiza-ya-matibabu-kwa-maji-ya-moto-kunywa.html

https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/153238-faida-za-kiafya-za-kitunguu-swaumu-garlic-featured.html
 
Last edited by a moderator:
Mh. waziri, sasa naona unanitisha kwani upara wangu nimerithi toka kwa wajomba ila baba yangu alikuwa na nywele nyingi sana. Swali, je nina uwezekano wa kupata haya matatizo ya moyo?

Mkuu kwa mujibu wa huu utafiti uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo ni mkubwa sana,wewe jiandae kwenda Hospitali ya Apolo iliyopo Hydrabad inchini India!
 

da hii kali he he he he kwani vibamia haviingii kunako??
 
Ni kweli. Inapunguza risk kwa kiasi fulani kwa sababu michubuko inakuwa kiasi.

Cc Madame B

Sasa itabidi tuanze kuulizana ili tuepuke hizo risk, mwenye kibamia atoke na mwenye uwanja mpana.....
 
Last edited by a moderator:


Mh. waziri. Nilifuata ushauri wako mara ya kwanza nilipoona ule uzi wako, ila tatizo linakuja pale ninapokula kitunguu swaumu. Yaani kina niwasha hufidhi na kunisisimua mishipa mwilini. Mara ya kwanza yaani kidogo nijipeleke hospitali jinsi nilivyopaliliwa na kile kitunguu.
 
kiponde ponde hicho kitunguusaumu kiwe laini kimeze kwa maji tosha kabisa kula asu buhi na usiku kila siku punje 1 tosha kabisa Mkereketwa_Huyu
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli. Inapunguza risk kwa kiasi fulani kwa sababu michubuko inakuwa kiasi.

Cc Madame B

Yaani japo nimechelewa kuiona Copy yako mndele wangu King'asti,.....lakini uko sahihi.
Vibamia havihusu babu weeeeeeeeeee..........
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…