Upasuaji wa haraka: Mtoto ameviringisha kitovu shingoni

tembaisdor

Member
Joined
Sep 19, 2011
Posts
29
Reaction score
8
Msaada:

Dada yangu ni mjamzito miezi tisa sasa, juzi kafanya utra sound wanasema mtoto amevingirisha kitovu shingoni kwa hiyo uwezekano wa kujifungua kawaida haupo ila kwa operation mapema bila hivyo mtoto atatoka amekufa.

Leo kaambiwa operation ifanyike kesho au Jumamosi hapo kwa Kairuki. Je, hii ni kawaida au ushauri tufanyaje?

Dada yeye mzito kuamua anaona ni afadhali ajifungue kawaida, wataalam tushaurini tafadhali.
 

Pole, je dada wako ana umri gani, mimba hii ni ya ngapi na mara ya mwisho kusikia mtoto akicheza tumboni ni lini? Pili, Ultrasound alifanya wapi?
 
Hapo ni kujifungua kwa operation tu sijawai ckia case ya ivyo mtu akajifungua kawaida.
 
Dada ana miaka 35, ni mimba ya mtoto wa pili, mtoto anacheza, utra sound kapiga hapo hapo kairuki
 
Hapo ni oparesheni tu. Mim mwenyew nisha pata kesi kama hiyo.awe jirani na jospitali kwa msaada wa madactari. Pia maombi yanatakiwa saana. Mungu amtie nguvu.
 
Mkuu poleni sana! Tatizo kuna baadhi ya hospital na madaktari hupenda kulazimisha kisu for higher commission.

However, kwa case yako huwa inatokea kupigwa kisu but mi Nina mtu alekuwa na Ishu kama hiyo, at the end hakupigwa kisu, alijifungua salama Aga Khan!
 
Iinategemea, mtoto akijiviringisha kitovu kwanza usalama wake unaweza kuwa mdogo sana kama hakuna wakunga wazoefu. Lakini kwa hospitali zetu hizi afanyiwe upasuaji tu ili kuavoid risk.
 

Mkuu fata ushauri wa madaktari kwani ukitaka ufate ushauri wa mkunga wa jadi (kama mawazo ya dada ako) basi mambo yakienda kombo mtajuuuuta.
Ishu ya kujifungua kwa mama ni "very sensitive case". Kimbieni hosp mapema .
 
Dada yangu pia alishawahi kukutana na case kama hiyo akawa mbishi kufanya operation akawa anamatarajio itakuja kuwa poa.At the end hakuna kilichobadilika na aliishia kufanyiwa operation na mtoto alisurvive kwa siku mbili tu akafariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…