king Mazee
New Member
- May 10, 2024
- 3
- 0
Katika Maisha ukikosa mwanzo mzuri basi kila kitu kitayumbayumba mpaka kisimame inahitajika kazi ya ziada kwakuwa chochote kile kikianza na msingi mzuri uwezo wa kustawi ni mkubwa maana watu husema , Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mmea ili ustawi vizuri lazima uanze na mizizi. Ili nyumba iwe bora ni lazima msingi wake uwe imara.
Katika Elimu yetu hapa Nchini kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana kuwa na wimbi la wasomi wengi kutokuwa na ajira lakini malalamishi haya yamekuwa nisehemu ya Maisha yaani kumekuwa na hali hiyo huku walioko Masomoni ni wengi na wanaohitimu ni wengi, wanao maliza Darasa la Saba huku hawajui kusoma wala kuandika, wanaomaliza ngazi mbalimbali za Elimu huku hawajui kuongea Kiingereza ipasavyo ni wengi.
Sasa inaonesha dhahiri kuwa idadi kubwa ya wasomi wengi wanao maliza au wanao hitimu Masomo yao wanaonekana hawana sifa ambazo walitakiwa wawenazo kulingana na viwango vyao vya Elimu, yaani mtu anamaliza Elimu ya juu kabisa lakini kwenye utendaji kazi unakuwa hauendani na kiwango cha Elimu aliyonayo.
Tatizo sio yeye tatizo ni kwenye chanzo Mfano kumekuwa na Wanafunzi ambao wanamaliza Elimu ya kidato cha Nne na kujiunga na Taasisi na Vyuo mbalimbali vya Elimu hapa Nchini na wanapohitimu Masomo yao tayari kwa kupangiwa maeneo ya kazi tena wanapelekwa Shule za Misingi walio wengi ambako ndiko Chanzo che Elimu ya Nchi hii kinapoanzia.
Neno la Mungu linasema katika kitabu cha Nabii Isaya 9:16 kuwa “ kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia”.
hapo tunasema usipoziba ufa lazima ujenge ukuta na Miaka mingi sasa ufa haujazibwa na ukiendelea kutozibwa na kujenga ukuta itahitajika nguvu ya kujenga Nyumba nzima ambayo inahitaji gharama kubwa zaidi.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiamua kufanya mabadiliko yafuatayo katika ajira tunaweza kujikuta mahali salaama kuanzia sasa hadi Miaka 25 ijayo na zaidi ya hapo ;
Kuajiliwa watu wenye viwango vikubwa vya Elimu katika ngazi ya chini ya Elimu (shule za Misingi)
Hapa nazungumzia watu wenye Elimu ya juu kabisa kuanzia ngazi ya Shahada nakuendelea, kuna mifano mingi ambayo inaonesha kabisa kuwa kukiwa na mabadiliko kwenye kuajili watu wenye taaaluma ya juu kufundisha viwango vya chini vya Elimu yaani madarasa ya chini kabisa mtu anapoanza kupata Elimu, kwa Mfano kuna jambo la kujiuliza na kupima hapa kuwa ni mara ngapi mtu anaenda katika vituo vya Afya au Taasisi yoyote ile ili apate huduma na kukuta kuna mtoa huduma wa ngazi ya chini yaani amemaliza tu Elimu ya Kidato cha Nne na kuchukua cheti tayari kuajiliwa, na ni mara ngapi mtu anapoenda sehemu za aina hizo akute mhusika ni mtu ambaye ana ngazi kubwa ya Elimu, nafikili kuna tofauti kubwa katika uwajibikaji wake , wengi wao kama ni Mzazi amempeleka Mtoto Shule na akamkuta Mwalimu Mkuu kuna namna anajisikia katika huduma ambayo atapewa, nzuri na bora ukilinganisha na angemkuta ambaye amemaliza tu Kidato cha Nne na kuchukua cheti na kuwa Mwalimu
Kuajiliwa watu wenye Elimu ya juu ya Saikolojia katika ngazi ya chini ya Elimu
Kwakuwa watu hawa wamekuwa wataalamu basi ni dhahiri kabisa kwamba wataweza kutambua Watoto kuwa huyu ni wa aina gani na huyu ni wa aina gani na kufanya wepesi ambapo watawajengea Watoto kujitambua angali mapema kuwa wao ni watu wa aina gani na kila Mtoto atakuwa na uelewa wa kuwa yeye anavyojiona anatakiwa awe Mtu flani hiyo ni baada tu ya kuwa na Waalimu ambao ni sahihi katika ngazi sahihi na wakati sahihi. Hii itapunguza hali ya kutokujielewa, mfano eti kwamba mtu anasoma kuanzia Darasa la kwanza mpaka anakaribia kujiunga na chuo na ndipo anaanza kuulizia kuwa hivi asomee nini jambo ambalo ilibidi alitambue angali yuko Shule ya Msingi
Kupewa Mishahara inayoridhisha na inayokidhi Mahitaji kwa watakao ajiliwa katika ngazi hiyo ya Elimu
Katika mambo yanayoibua nguvu ya kufanya kazi mbali na wito, ni malipo mazuri yanayoridhisha, ikiwa waajiliwa hawa watapewa na kulipwa Mishahara inayoridhisha kwa kutambua mchango wao katika kujenga Taifa lenye watu wanaojitambua, wabunifu, wanao fanya kazi kwa bidii, waadilifu na kadhalika ni muhimu wapewe na walipwe kwa namna ambavyo wanastahili, kupewa na kuandaliwa Mazingira mazuri ya kuishi pia.
Kwakuwa watoto watakuwa wamefundishwa vyema na inavyotakiwa , ndipo tutaona matunda yake kwakuwa mizizi iimara na matawi sasa yatachanua, yaani katika Nyanja zote na Sekta zote kutakuwa na watu wengi wanaostahili kuwepo katika Nyanja hizo na Sekta hizo .
kwahiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwekeza kwenye chanzo ambako ndiko kuna kazi kubwa na ndiko utaratibu huanza kwakuwa Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na wanasema siku zote kuwa samaki mkunje angali mbichi na Serikali ihakikishe hili zoezi linafanyika kwa Shule zote yaani za Serikali na Binafsi.

Upvote
1