Mboji ni aina ya mbolea ya asili yenye rangi nyeusi kahawia na harufu nzuri ya kidongo ambayo hutokana na kuoza kwa mchanganyiko wa masalia ya mimea,mazao au matunda, kunakosababishwa na vijidudu na wadudu rafiki wa mazao.
Mbolea ya mboji unaweza kutengeneza mwenyewe kwa kukusanya mabaki ya mimea na matunda kisha kukauka juani na kuchekechwa katika chekecho lililotengenezwa kwa wavu kama vile unachekecha mchanga au udongo ili kuisafisha kwa kuondoa vipande vya miti ambavyo havijaoza. Ikiwa mahitaji yako ya mbolea ni makubwa unaweza kununua kwa wazalishaji waliojikita kwanye uandaaji wa mbolea ya mboji.
Namna ya kutumia mbolea ya mboji
Mboji huweza kutumika kama mbolea kwa sababu ina virutubisho muhimu kwa ukuaji wa mmea katika viwango tofauti hasa virutubisho vya msingi vya Naitrojen, Fosfati na Potashi (N.P.K). Mboji kama mbolea huweza kutumika hata kabla ya kuiva vizuri kwa kuwekwa juu ya udongo kuzunguka shina la mmea au ikiwa imeiva kwa kuichanganya na udongo katika shamba zima au katika mashimo ya kupandia. Mara nyingi ni vigumu kutengeneza mboji yenye wingi wa kutosha kusambazwa shamba zima hasa lenye ukubwa wa ekari moja au zaidi hivyo ni busara kuweka mboji kama mbolea katika mashimo ya kupandia.
FAIDA ZA MBOLEA YA MBOJI
Mboji kifusi cha tani moja ni 350,000/=
Mboji iliyopakiwa kwenye mifuko kwa idadi ya tani moja ni 400,000/=
Mpiji Magohe
0699494650
N.B: Gharama za usafirishaji inategemea na idadi ya tani unazochukua na mahali zinapoenda , kwa kuanzia tani 6 na kuendelea tutachangia usafirishaji kukufikishia mzigo popote.
Upatikanaji wa mbolea unaweza kuchukua hadi siku 7 kutegemeana na wingi wa order.

- Uandaaji wa mbolea ya mboji hauna gharama na ni rahisi hivyo wakulima wa ngazi zote wanaweza kuumudu.
- Mbolea ya mboji huboresha muundo wa udongo unaopelekea kuwa na mzunguko mzuri wa hewa na maji katika udongo.
- Mbolea ya mboji huongeza virutubisho vinavyohitajika na mmea katika udongo na hivyo kuongeza mazao.
- Mboji huongeza uwezo wa udongo kutunza maji na hivyo kupunguza kasi ya ukaukaji wa udongo hasa katika maeneo yenye hali ya joto na yasiyopata mvua za kutosha.
- Mbolea ya mboji huweza kutumika kama mbadala wa mbolea ya samadi wakati wa kuandaa kitalu cha mboga.
- Mbolea ya mboji huboresha afya ya mmea na kufanya uwe na uwezo wa kustahimili magonjwa.