Upatikanaji wa mbuzi aina ya Boer hapa Tanzania

Upatikanaji wa mbuzi aina ya Boer hapa Tanzania

bbiswalo

New Member
Joined
Jun 28, 2021
Posts
3
Reaction score
4
Nimekuwa nikipata maswali mengi kutoka kwa wadau wa ufugaji mbuzi ambao wanaotaka kujua kuhusu upatikanaji wa mbuzi aina ya Boer hapa Tanzania.

Ili kujibu swali hili nimetengeneza video ambayo inatoa taarifa ya kutosha kuhusu upatikanaji wa mbuzi aina ya Boer hapa Tanzania .

Hebu angalia video kwenye hii link hapa chini na kama bado una maswali usisite kuwasiliana nasi.

F1213C50-3FFF-4A03-A3B3-D4726009E64F.jpeg
 
Presenter ktk video hatoi maelezo yenye msaada.

Alichotakiwa kueleza ni PROCESS ya kuagiza mbuzi wa Boer kwa wale wenye mahitaji nao.

Awape wananchi CONTACTS za wauzaji wa mbuzi hao South Africa au Namibia ili watu wajiongeze.
 
Ni jambo la kushangaza sana kuwa hawa mbuzi wamekuwa kama madawa ya kulevya

Yaani swala anapelekwa Dubai na wasiokuwa raia ila kuleta mbuzi Bongo imekuwa mbinde
Kila wakati naona watu wanaulizia hao mbuzi mbona Jirani Kenya wamejaa?
Tunakwama wapi?
 
..Mbogo Ranches nasikia wanasaidia wafugaji wadogo kuagiza mbuzi pure boer kutoka afrika kusini.

..labda watu wajiunge kikundi wafugaji watatu au watano wawatumie Mbogo Ranches kuagiza beberu mmoja mna-share.

www.instagram.com/mbogo_ranches
www.estates.co.tz

Cc wakaliwetu, Manchid
Nikweli kabisa wale jamaa wanasaidia sana tena ukipitia hao unapata kitu cha maana sana maana wanafwata njia za kitaalamu zote za kumpima Mbuzi kabla hajaanza kusafirishwa. Wa south wanaitunza hiyo mbegu vyema kwahuyo wakati wakuuza wanajitahidi sana wauze Mbuzi mwenye ubora kabisa ili wasijiharibie soko lao. Kumbuka ukitaka kufuga Boer unapashwa kujiandaa kwanza kabla ya kumwagiza na kumleta hapo unapotaka kufugia.
 
Presenter ktk video hatoi maelezo yenye msaada.

Alichotakiwa kueleza ni PROCESS ya kuagiza mbuzi wa Boer kwa wale wenye mahitaji nao.

Awape wananchi CONTACTS za wauzaji wa mbuzi hao South Africa au Namibia ili watu wajiongeze.
Video kama title yake inavyosema ni kuhusu upatikana wa mbuzi aina ya Boer hapa Tanzania na sio upatikanaji wa mbuzi South Afrika. Pale watu watakapotaka kujua process ya kuagiza mbuzi South Afrika watapewa hayo maelezo wakiyaomba. Si rahisi kukidhi mahitaji ya kila mtu kwenye video moka. Mwingine anataka kujua jinsi ya kuwapata hao Boer Kenya au Uganda, na mwingine kutoka Zambia.
 
Nikweli kabisa wale jamaa wanasaidia sana tena ukipitia hao unapata kitu cha maana sana maana wanafwata njia za kitaalamu zote za kumpima Mbuzi kabla hajaanza kusafirishwa. Wa south wanaitunza hiyo mbegu vyema kwahuyo wakati wakuuza wanajitahidi sana wauze Mbuzi mwenye ubora kabisa ili wasijiharibie soko lao. Kumbuka ukitaka kufuga Boer unapashwa kujiandaa kwanza kabla ya kumwagiza na kumleta hapo unapotaka kufugia.
Na karibuni Mbogo sasa wataanza kuuza Boer ambao wamewazalisha wenyewe hapa Tanzania. Hii itasaidia sana wafugaji ambao hawana uwezo wa kwenda South Afrika kuleta hawa mbuzi. Na tayari wameshaanza kuuza mbuzi chotara wa kienyeji na Boer.
 
Video kama title yake inavyosema ni kuhusu upatikana wa mbuzi aina ya Boer hapa Tanzania na sio upatikanaji wa mbuzi South Afrika. Pale watu watakapotaka kujua process ya kuagiza mbuzi South Afrika watapewa hayo maelezo wakiyaomba. Si rahisi kukidhi mahitaji ya kila mtu kwenye video moka. Mwingine anataka kujua jinsi ya kuwapata hao Boer Kenya au Uganda, na mwingine kutoka Zambia.

..nadhani wengi wangependa kujua process ya kuagiza boer hatua kwa hatua.

..hakuna video inayotoa elimu hiyo popote pale.
 
Hawa mbuzi soko lake litakuwa. wapi? Mbuzi auzwe laki 7?
 
Na karibuni Mbogo sasa wataanza kuuza Boer ambao wamewazalisha wenyewe hapa Tanzania. Hii itasaidia sana wafugaji ambao hawana uwezo wa kwenda South Afrika kuleta hawa mbuzi. Na tayari wameshaanza kuuza mbuzi chotara wa kienyeji na Boer.
Jambo la kumshukuru Mungu kwa kuwa na hawa jamaa ktk huu ufugaji.
 
Kuna Mdau ngoja nimuulizie ana connection za waagizaji, ila wake anadai aliagizia kupitia Kenya tena mwaka huu huu
 
..Rwakita Agri and Vet Services yuko hapo kwenye video.

..anasema ni agent wa kuagiza ng'ombe wa kisasa toka Kenya.

..kama anaweza kuagiza ng'ombe huenda anaweza kuagiza na mbuzi.

..ametoa mawasiliano yake ya simu , +255 713 178 868.

..binafsi sijawahi kumtumia, kwa hiyo atakayewasiliana naye aje atupe mrejesho kama ni muaminifu au la.

... nahitaji wale ng'ombe wa Museven pembe futi 5 nawapataje wadau?
 
Hao ng’ombe wanapatikana sana mkoa wa geita na kagera wanaitwa nyankole. Best kwa nyama na wana kilo nyingi .changamoto ipo kwenye kuwafuga hawahimili ukame hata kidogo majan makavu hawal
 
Back
Top Bottom