SoC02 Upatikanaji wa mlo kwa Wanafunzi shuleni

Stories of Change - 2022 Competition

Proporis

Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
12
Reaction score
7
UTANGULIZI

Injini yoyote ili ifanye kazi inahitaji mafuta ya kuiendesha na kuirainisha, hii ni sawasa na mahitaji ya mwili. Mwili ili ufanye kazi unahitaji upate chakula kwa matumizi mbalimbali. Mwili unapopata chakula unaruhusu viungo vyote vya mwili kwa umuhimu wake kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ubongo.

Ukosefu wa mlo shuleni umechangia kwa asilimia zaidi ya 30 kutokufanya vizuri kwa wanafunzi wengi wa shule za kutwa hasa za msingi na sekondari zilizo umbali mrefu kati ya kilomita 8 mpaka 10 kutoka nyumbani. Pia ukosefu wa mlo umechangia kuchochea tabia nyingine hatarishi kwa wanafunzi kama wizi, mimba utoro na kujichukia. Wanafunzi wengi wanaotokea kwenye kaya zenye kipato kidogo wanakutana na ukosefu wa mlo wa asubuhi, mchana na wakirudi nyumbani jioni wanapata mlo wa usiku ambao haukidhi mahitaji yao ya mwili. Katika kutatua changamoto ya njaa mwanafunzi uanza kupitia matunda na mazao yanayo lika kirahisi kama mihogo n.k. Pamoja na hayo wengine uanzisha tabia za udokozi ili kuweza kujipatia ela ya kununua chochote wawapo njiani kuelekea shuleni au wanapo rudi nyimbani. Wale wanaopewa nauli udiriki ata kula nauli kisha kutembea au kucholewa kuondoka vituoni wakitegemea misaada ya lifti au kuomba nauli kwa wasamalia wema. Mabinti wamekua wakiangukia katika mikono ya vijana au watu wazima kwa matarajio ya kusaidiwa mahitaji hasa chakula hali maarufu chips.

Ukosefu wa chakula kwa wanafunzi pamoja na kuwachochea kuingia katika tabia hatarishi zinazo dumaza ustawi wao wa maisha pia ukosefu wa chakula unapeleka kuathiri mfumo wa kujifunza na ujifunzaji. Umakini na utulivu unapotea kwa sababu ya njaa sambamba na upokeaji wa mafunzo ulio hafifu. Kufikiri na kuchanganua mambo unaingiliwa na mwanafunzi kupunguza kuona au kuyapa umuhimu masomo. Jambo linaweza kuonekana kwa udogo maana umkuta mtu mmoja mmoja lakini matokea ya jumla uonekana katika matokeo yao ya mwisho ya masomo na majanga mengine mbalimbali.

Ni ukweli wa wazi kwamba kuna kaya nyingi ambazo kipato ni kidogo kumudu mahitaji ya familia pamoja na mlo ni changamoto. Shule zetu za msingi na sekondari hasa za kutwa pia hazimudu kutoa mlo wa asubuhi na mchana kwa wanafunzi, ata kwa yale madarasa ya mitihani yanayo ongezewa muda wa ziada kwa ajili ya kujifunza. Pamoja na kwamba kuna shule ambazo zimeweka mpango kwa makubaliano na wazazi bado pia kua kaya hazimudu kuchangia na wengi wanaweka ubishi kwa kitokuona umuhimu wa mlo wa mwanafunzi akiwa shuleni. Mzigo wote unazilemea kaya zilizo tayari kuchangia. Pia kuna sehemu nyingine mpango umeshindikana kwa sababu ya ugumu wa wazazi kuchangia na kaya kuwa na kipato kidogo.


NINI KIFANYIKE

1. Shule ambazo ziko maeneo ya mijini au senta waibue vyanzo vya mapato kupitia maeneo ya shule zao mfano ujenzi wa kumbi za mikutano, vibanda vya biashara au viwanja vya michezo. Mapato yanayo patikana wawapitie wanafunzi chakula kutokana na kipato.

2. Shule zilizo nje ya mji miundombinu ipelekwe na upimaji wa maeneo ufanyike kupanfisha hadhi eneo husika ili kiweza kuuza yanzo mbalimbali vya mapato vitakavyo ibuliwa na wanafunzi watapata mlo kutokana na mapato yatakayo patikana

3. Shule ambazo zimezungushiwa kuta zinaweza kufanywa vibanda palipo na uwezekano

4. Maeneo ya vijijini na kwenye kata, maeneo yatambuliwe na kukodishwa kwa wawekezaji walio tayari kufanya uwekezaji wa kilimo au shughuli rafiki kwa mazingira ya shule na mapato yaka nunua chakula kwa wanafunzi

5. Shule yenyewe inaweza kuanzisha uwekezaji wa kilimo biashara cha mda mrefu kama katani, miembe, michungwa n.k kutegemea na jiografia na ukanda wa mazao kustawi. Au mazao ya muda mfupi kama alizeti, ufuta n.k

UTEKELEZAJI

1. Shule zenye vyanzo vya mapato vielekeze mapato yake katika kutatua tatizo la njaa kwa wanafunzi kwa kuwapatia mlo, mmoja au miwili.

2. Shule ambazo zinavyanzo na zilikua hazija anza kutumia vyanzo hivyo viandae na kupanga namna nzuri ya kutumia vyanzo hivyo kujipayia kipato kwa ajili ya mlo kwa wanafunzi.

3. Shule zihusishe wadau mbalimbali wa kimaendeleo katika maeneo yao na serikali kuwezesha hatua za kwanza za uwekezaji na baade miradi ikisha imarika basi wanaendelea nayo.

4. Wachumi na wanamipango wa sekta mbalimbali wahusishwe katika kulichakata na mwisho kupata mpango endelevu wenye tija

5. Kata ambazo hazina maeneo ya uwekezaji ya vijana lakini zina shule zenye maeneo makubwa wapewe vijana kupitia mipango na miradi mbalimbali ya uwezeshaji na uwekezaji wayatumie, mapato yatakayo patikana kaisi yarudi shuleni.

6. Kamati thabiti zenye wadau wa amendeleo na wazazi ziundwe kusimamia ufanisi wa zoezi ilo.

HITIMISHO

Uwepo wa vyanzo mbalimbali vya mapato vitokanavyo na shule vitapunguzia mzigo kwa wazazi, shule na serikali katika uendeshaji wa taasisi hizo hasa katika matatizo madogo madogo na makubwa kama ukosefu wa chakula kwa wanafunzi. Pia kama itakua ni shughuli inayo fanyika palepale shuleni kwa kushirisha wanafunzi basi itakua ni chachu ya wanafunzi kupata elimu ya kujitegemea kupitia utekelezaji na uendeshaji wa miradi hiyo. Wanafunzi wanaweza kutengewa saa moja kila siku kwa ajili ya kupata mafunzo ya ziada wakishiriki utekelezaji wa miradi na kujipatia maarifa mbalimbali

##Karibu upige kura yako na pia tujadiri##
 
Upvote 2
Karibuni wadau tusome na kupigia kura, tupush agenda umuhimu wa mlo kwa wanafunzi, wadogo zetu na wanetu.
 
Sawa mkuu ila mambo ya shuleni hasa sekondari inategemeana na uelewa wa wa jamii husika... kuna maeneo ni pasua kichwaa
 
Sawa mkuu ila mambo ya shuleni hasa sekondari inategemeana na uelewa wa wa jamii husika... kuna maeneo ni pasua kichwaa
Shule kupitia kamati zake wakija na maazimio nq yakapitiwa na viongozi wa serikali kwa maboresho na taratibu zote muhimu zikafuatwa nina uhakika wazazi watalipokea vizuri tu ukizingatia ni kwa maslahi ya watoto wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…