SoC04 Upatikanaji wa taulo za kike(ped) bure kwa mabinti mashuleni

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 4, 2024
Posts
13
Reaction score
21
Upatikanaji wa Taulo za kike (ped) bule Kwa mabinti kuanzia shule za msingi Hadi kidato cha Sita
Serikali haijaingiza swala la upatikanaji wa Taulo za kike Kwa wanafunzi kama kipaumbele kimojawapo cha Afya kwenda sambamba na Elimu inayotolewa bule

UTANGULIZI
Swala la hedhi nila kibiolojia ni Afya Kwa mwanamke, mwanamke ambae umli wake unamruhusu apate hedhi na hapati basi huyo anamatatzio ya kiafya. Jamii ya sasa ina uelewa mkubwa kuhusiana na swala la hedhi na sio sili tena hivyo basi ni swala la msingi na la muhimu Kwa Afya za watoto wetu ambao ni jamii ya kesho Jambo hili linagusa kila mtu kwasababu kila mtu anahusiana na mwanamke Kwa kua mama, mke, mtoto, dada, shangazi na Bibi.

Serikali haina budi kuanda sera ya upatikanaji wa Taulo za kike Kwa shule za msingi Hadi kidato cha Sita. Kama zilivyo sela za ukimwi upatikanaji wa kondom bule, sela za uzazi wa mpango bule, sela ya kuzuia na kupambana na malaria bule, sela za kuwasidia watu walio athirika na madawa ya ulevya, vivyo hivyo upatikanaji wa taulo zakike unahitajika kwa kiwango kikubwa katika shule nyingi haswa kwa mashule yanayopatikana vijijini.

Hedhi sio swala la hiari Kwa mwanamke /msichana ni swala la lazima hivyo Serikali inapaswa kulichukulia Kwa jiicho tofauti iingizwe Sera ya Afya itakayo tekekezwa bure kama zilivyo sela nyingine ili kumlinda na kusaidia binti ambae hawezi kumudu gharama za kununua Taulo za kike kila mwezi

Kwa mfano binti anae toka Kaya masikini ambayo mlo mmoja Kwa siku ni shida, je anawezaje kumudu gharama za Taulo za kike kila mwezi ambazo Kwa bei ya mtaani ni TSH 3000

UTEKELEZAJI WAKE
Serikali unaweza kuweka Taulo za kike kama bidhaa ya Afya ambazo zinatolewa bule kwenye hospital pamoja na vituo vya Afya Yani VERTICAL PROGRAM nchi nzima ambazo zitakuwa sambamba na bidhaa kama TB program, HIV kondomu na ARVS, malaria program ambapo wanafunzi wanaweza kwenda kwenye hospital au zahanati iliyo karibu kuchukua kila mwezi kama wanavyofanya kwenye bidhaa zingine za afya ikiwemo dawa za kufubadha vvu

Programu ya usambazaji katika shule zote kwakutumia maafisa Elimu kulingana na idadi ya wanafunzi wakike katika eneo husika

Kutumia watendaji na wenyeviti kusambaza katika mashule ilikufikia watoto WA Kaya zilizo jificha

Kusambazo Taulo hizi Kwa makundi maluumu ya wasichana wenye ulemavu katika shule zao

UPATIKANAJI WA FEDHA KATIKA WIZARA HUSIKA
Matumizi ya bucket fund kama ambavyo bidhaa za afya nyingine zinazotolewa bule, Serikali inahitajika kuongeza basket fund Kwa kila kituo cha Afya kinachotoa Taulo hizi zakike

Wafadhili mfano UNICEF na WHO kupunguza Kodi au ifutwe kabisa Kwa bidhaa hizi ilikuruhusu kampuni nyingi kuingiza nakusadia Serikali

Ubunifu WA upatikanaji WA fedha kama kutoza angalau Tsh 10 Kwa kila laini Kwa mwezi ilikuchangia upatikanaji WA Taulo hizi Kwa mabinti Mashuleni

FAIDA KWA JAMII NA SERIKALI
Kupunguza utoro na kuongeza maudhurio hasa katika siku ambazo binti ankaua kwenye hedhi, Kwa mwanamke/msichana ambae Afya yake iko vizuri (physiology) anaingia hedhi siku 5-6 hivyo basi kama anapata changamoto ya Taulo za kike kila mwezi anakosa masomo siku 6 ambapo Kwa mwaka katika miezi 10 ya masoma anauwezekano wakukosa masomo siku 60 na Kwa mwanafunzi wakidato cha nne Kwa Miaka yote mi nne atakosa masomo kwa siku 240



Chanzo cha picha ni Kwa hisani ya Milardayo​

Kua na hedhi salama kunafanya kujiamini Kwa wasichana mbele ya JAMII kupunguza nakuondoa magonjwa kama ya njia ya mkojo na Tumbo.

Kupunguza maambukizi ya vvu haswa yatokanayo na vishawishi vya kukosa mahitaji ya Taulo za kike ambapo kaundi hili la mabinti liko kwenye hatari kubwa ya maambukizi kutokana na takwimu za mwaka huu 2024 ambapo kupitia tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania, TACAIDS kundi la wasichana Kati ya Miaka 15-24 limethibitika kuongoza Kwa maambukizi katika kundi hili wengi ni wasichana wa shule uwepi wa taulo za kike mashuleni utapunguza kundi hili kupata vishawishi.

Picha Kwa hisani ya JAMIIFORUMS

Kujenga jamii inayo thamini na kuelewa maswala ya hedhi salama na kujenga jamii itakayo walinda nakuwathamini mabinti

HITIMISHO
Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu aliitaka jamii na wadau kuweka mazingira rafiki kwenye suala la hedhi salama ili mabinti hususani WA shule wawezekutumiza majukumu Yao bila vikwazo
Waziri Ummy alitoa wito huo mei 22,2024 Jijini Dodoma wakati akitoa Tamko Kwa umma kuhusu maadhimisho ya wiki ya hedhi salama

Bila hedhi salama hakuna ustawi, Kwa nini tuone kinyaa kuzungumzia masala ya hedhi salama alihoji Waziri Ummy na kusema, suala la hedhi salama hutuwezi kulikwepa ni sehemu ya kuendeleza kizazi katika jamii na Taifa Kwa ujumla alisisitiza Waziri Ummy

Ni muda muhimu sasa kwa Serikali kufanya swala la hedhi kua swala la kisela na kuliweka kwenye utekelezaji na kuweka bajeti ili kuweza kuwasadia mabinti Mashuleni kwa kufuata mikakati hapo juu

 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…