UPDATE: Aliyedaiwa kuua watu na kusababisha Mechi ya Ubelgiji vs Sweden kuahirishwa, auawa na Polisi

UPDATE: Aliyedaiwa kuua watu na kusababisha Mechi ya Ubelgiji vs Sweden kuahirishwa, auawa na Polisi

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
IMG_4739.jpeg

IMG_4740.jpeg


Mtu huyo aliyetajwa kama Gaidi, aliwapiga Risasi Raia wawili wa Uswidi na kumjeruhi mmoja kabla ya mechi ya Ubelgiji ya kufuzu #Euro2024 dhidi ya Uswidi jijini Brussels ameuawa wakati tahadhari ya Ugaidi ikitangazwa kwa kiwango cha juu zaidi
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Annelies Verlinden, amesema mtuhumiwa ametambuliwa kwa jina la Abdesalem L (45) raia wa Tunisia na Silaha inayoaminika kutumika katika mauaji hayo pia, imepatikana
1697530578975.png

===========

Mchezo wa kufuzu Euro 2024 kati ya wenyeji Ubelgiji dhidi ya Sweden umeshindwa kuendelea kipindi cha pili baada ya mashabiki wawili wa Sweden kushambuliwa kwa risasi na kuawa.

Tukio hilo limetokea katika Mji wa Brussels, Ubelgiji ulipokuwa ukifanyika mchezo huo leo Oktoba 16, 2023.

Wachezaji wa Sweden, waligoma kurejea kipindi cha pili kuendelea na mchezo huo baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Taarifa za awali zinadai kwamba, mshambuliaji katika tukio hilo anahusishwa na Kundi la ISIS.

Wakati mchezo huo ukiahirishwa, matokeo yalikuwa sare ya goli 1-1.
 
Hawa wenye misimamo mikali ukiwakamata sio wa kuwaua kwa risasi ,dawa yao wauliwe taratibu kwa kukatwa vipande vya sehemu za mwili au viungo
 
HIVI ALBADIRI AU MAJINI HAYAWEZI KUPAMBANA NA ADUI ZENU?
KWA NINIMTUMIE SILAHA YA MZUNGU?
 
Back
Top Bottom