TZ-1
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 4,321
- 7,501
Wadau wa mazao msimu wa korosho umeanza na umeanza vzr , nazn n vyema tukatumia forum hii kupeana update huko mnadani nini kinaendelea
Naomba taarfa za bei za minada ziwe rasmi kuepusha mislidi
Mnada wa kwanza wa msimu mpya wa korosho mwaka 2024/2025 umefanyika leo October 11,2024 katika Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara, ukisimamiwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), huku bei ikipanda hadi kufikia Tsh. 4120 kwa kilo moja.
Mnada huo umeshuhudia kilo moja ya korosho ikiuzwa kwa bei ya kati ya Tsh. 4,120 bei ya juu na 4,035 bei ya chini.
Chama Kikuu cha Ushirika kinachohudumia Wilaya za Newala na Tandahimba (TANECU) kimepeleka sokoni jumla ya tani 3,857 za korosho katika mnada huo, ambazo zote zimenunuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ambaye ndiye Mgeni rasmi katika mnada huo, amesema huo ni mwanzo mzuri ambao unaonesha kuwa msimu wa korosho 2024/2025 utakuwa wa manufaa kwa Wakulima.