Wakulima wa zao la korosho wa Tandahimba na Newala kupitia chama kikuu Cha ushirika Tanecu Ltd wameuza korosho zao kwa bei ya juu ya sh 3430 na bei ya chini ya sh .3200 katika mnada wa tatu wa zao Hilo uliofanyika Leo October 25 2024 katika ukumbi wa zamani wa halmashauri ya wilaya ya Newala uliopo halmashauri ya mji Newala
Akitangaza bei hizo mwenyekiti wa Tanecu Ltd Karim Chipola amesema wao kama wasimamizi wa mkulima watahakikisha korosho zote zinazopelekwa ghalani zinauzwa hivyo amewataka wakulima kuzikausha vizuri korosho zao ili ziendelee kuwa Bora zaidi
Mnada huo umeendeshwa kwa mfumo wa mtandao unaosimamiwa na TMX ambapo korosho tani 19000 na kilo 73120 katika mnada huo zimeuzwa
Kwa upande wao wakulima walioshiriki mnada huo wamesema wanaridhishwa na bei hizo