Update: Zinakaribia saa 24 Mbagala hakuna umeme.

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Wakazi wa Mbagala jana kuamkia leo hawana umeme na sasa ni saa 8:19 hawana umeme ni kasoro saa tatu zitimie saa 24 za Tanesco kutokuwa na umeme.
 
Watoto wa sikuizi bwana....enzi zetu kulikuwa hakuna hata umeme, yani ni vibatari tu lakini tuliishi..Sasa wewe umeme siku moja tu ndio kelel zote hizo?
 
Unataka kuishi kama zamani? Unaona ni jambo la maana kusifia shida tulizopitia zamani?
 
Huwa nashangaa sana ni kwanini watu wanategemea sana umeme wa TANESCO hasa wale wasio kuwa na matumizi makubwa, hapa namanisha matumizi madogo ya nyumbani kama kuwasha taa, TV, redio na kuchaji simu. Ni kwanini watu wasinunue Solar na kuweka majumbani badala ya kutegemea huu umeme wa TANESCO ambao tangu nimejitambua haujawahi kuwa wa uhakika.

Mwanga tunao wa kutosha, bei za solar si kubwa kiviiile, ila bado unakuta mtu analia lia na umeme wa TANESCO. Nchi za ULAYA wameendelea na umeme haujawahi kukatika kizembe, ila utakuta nyumba nyingi tu zina Solar pia. Ila sie ....ngoja niishie hapa.
 
Acha kujiongelesha Mkuu. Kuunganisha tu umeme gharama yake inaweza isizidi 500,000, lakini hapa hapa Mjini "Daslamu" kuna watu wanaishi nyumba hazina umeme. Unafikiri wanapenda!? Ni umasikini wa kipato uliopitiliza. Sasa jiulize mtu huyo atamudu gharama za kuweka mfumo wa solar nyumbani kwake!? Maana unazidi hiyo 500,000.

Cha kuongezea, kuna mamilioni ya watu wanakaa kwenye nyumba za kupanga. Iwe nyumba nzima ya familia au nyumba yenye vyumba vya kupangisha. Hapo ni wazi suala la umeme wa Solar haliko mikononi mwao.
 
Watoto wa sikuizi bwana....enzi zetu kulikuwa hakuna hata umeme, yani ni vibatari tu lakini tuliishi..Sasa wewe umeme siku moja tu ndio kelel zote hizo?
Ukiona hivyo ujue hilo ni sukuma au wale marafiki zao wanatafuta support humu waanze kuiponda serikali iliyopo madarakani utafikiri wakati wa yule mungu wao umeme ulikuwa haukatiki.
 
Wachangiaji wote kuanzia namba 2 hadi namba 7 wanaonekana wana matatizo ya kifikra
 
Watoto wa sikuizi bwana....enzi zetu kulikuwa hakuna hata umeme, yani ni vibatari tu lakini tuliishi..Sasa wewe umeme siku moja tu ndio kelel zote hizo?
Usifananishe zama Mkuu . Utakuwa unakosea sana. Miaka ile kabla ya bodaboda nilikuwa natembea dakika 50 kutoka kituo cha daladala kwenda nyumbani kwa Dingi. Leo na wimbi lote la bodaboda itakuwa ni ufala eti niendelee kukanyaga kwa mguu.

Ongezea na hili, Hapo ulipo simu yako ina bando la dakika na internet. Lakini internet ikizingua hata kama simu za kawaida unapiga Lazima ukereke.
 
Acha kujiongelesha Mkuu. Kuunganisha tu umeme gharama yake inaweza isizidi 500,000, lakini hapa hapa Mjini "Daslamu" kuna watu wanaishi nyumba hazina umeme. Unafikiri wanapenda!? Ni umasikini wa kipato uliopitiliza. Sasa jiulize mtu huyo atamudu gharama za kuweka mfumo wa solar nyumbani kwake!? Maana unazidi hiyo 500,000.

Cha kuongezea, kuna mamilioni ya watu wanakaa kwenye nyumba za kupanga. Iwe nyumba nzima ya familia au nyumba yenye vyumba vya kupangisha. Hapo ni wazi suala la umeme wa Solar haliko mikononi mwao.
1. Umezungumzia umeme wa Solar ni gharama kuliko TANESCO. Nadhani bado hujapiga tu hesabu vizuri, umeme wa TANESCO utakuwa ni ghari kuliko wa Solar, nitakuelewa ukisema gharama za mwanzo za umeme wa Solar zinaweza kuwa kubwa kidogo ukilinganisha na umeme wa TANESCO. Japo napo inategemea maana ukilipia na nguzo gharama zinakuwa kubwa zaidi. Umeme wa TANESCO pamoja na kukatika kwake unalipia kila mwezi ambapo umeme wa Solar ukiweka ndio umeweka.

2. Jambo lingine chunguza hata hao wenye huo uwezo, wanaoishi kwenye mageti, unakuta hata wao wanategemea huo umeme wa TANESCO. Yaani umeme ukikatika na kwake panakua giza. Huyo nae utasema hana umeme wa Solar kwa sababu ya 'umaskini uliopitiliza' ?

3. Kuishi kwenye nyumba ya kupanga bado sio sababu ya kushindwa kuweka solar, bado unaweza kuongea na mwenye nyumba na ukaiweka hiyo solar yako. Siku ukihama, unahama nayo.
 
Tatizo kwenu mbagalaaa, hapa nyumba mbele jalala.

sema nin, shida ya umeme sio kitu kipya bongo mkuu.
 
Back
Top Bottom