Updates: Kinachoendelea kwenye Maadhimisho ya Miaka 50 ya Biashara Kimataifa Saba Saba Julai, 2026 Dar es Salaam

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Leo Julai 7, 2026 ni Maadhimisho ya Miaka 50 ya Biashara Kimataifa, maarufu kama Saba Saba (77), ambapo mataifa mablimbali hupata kuonyesha bidhaa zao na kuimairisha ushirikiano wa kibiashara na Tanzania.

Siku imeanza vizuri ikiwa na kimvua kwa mbaliiii, kushusha vumbi njia ionekane vizuri ili wananchi wapate kusherekea vizuri na kwenda kuangalia nini kipo 77 mwaka huu. Kama hujaenda siku za nyuma leo ni siku nzuri ya kwenda kwenye maonyesho hayo maana hali ya hewa inaashiria kuwa shwari, huenda kusiwe na joto kali.

Nimesikia safari hii kuna Maliasili wameleta tembo, ngoja tukaone kama mara hii wanawaweka wanyama katika mazingira mazuri au ili mradi pesa iingie kama miaka mingine bila kujali mazingira yao.

Mbali na hilo nna maswali kadhaa ya kwenda kuwauliza NIDA, Wizara ya Mambo ya Ndani, Polisi na wengine kadhaa kwenye my list, hopefully nitapata majibu kama Watanganyika wengine wanavyotegemea kupata majibu yaoπŸ˜‰πŸ€ͺ

TUKUTANE 77🫡🫡
 
Ko mali asili wamemleta
Harmonize a.k.a tembo
Diamond platnumz a.k.a simba
Rayvanny a.k.a chui
 
karibu sana mTanzania,
ukishindwa leo, unaweza kuja kesho au siku nyingine yoyote katika wiki, kwasababu maonyesho haya yatafungwa rasmi July 13.2026, yaani j3 ijayo njoo na familia yako πŸ’
 
karibu sana mTanzania,
ukishindwa leo, unaweza kuja kesho au siku nyingine yoyote katika wiki, kwasababu maonyesho haya yatafungwa rasmi July 13.2026, yaani j3 ijayo njoo na familia yako πŸ’
Mbwa mwitu na chui weusi watakuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…