Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,033
Reaction score
723


Leo ni August 1,2015 Wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima wanakusanyika katika maeneo ya matawi yao kuchagua mgombea mmoja atakayeshindana na wagombea wengine kutoka vyama tofauti na CCM.

Mchakato wa kampeini katika mkoa huu zimetawaliwa na vituko,udhalilishaji kwa baadhi wa wagombea hivyo hata upigaji kura za maoni utakuwa hivo hivyo,hii ndiyo sababu inatufanya tufuatilie live kura hizi.

Updates...






MORE UPDATES:







 
Kutoka Mkoani Kagera nakuletea LIVE UPDATES ikiwemo na matokeo kadri nitakavyoyapata.

Historia kidogo
Mkoa wa Kagera una majimbo tisa ya uchaguzi ambapo wabunge wawili tu wametangaza kung'atuka ambao ni Deogratias Ntukamazina wa Jimbo la Ngara na Bw Esutace Katagira wa jimbo la Kyelwa.

Saa 12:02 Adhuhuri
Hizi ni baadhi ya picha kutoka vituo mbalimbali katika kata zilizoko manispaa ya Bukoba.
wengine kutoka vyama tofauti na CCM.








Saa 10:38 Asubuhi
.Wanachama wa CCM wanaendelea na upigaji kura ingawa katika maeneo mbalimbali ya kata ya Kanyigo wilyani Missenyi wasimamizi wanalalamikia kuwepo kadi za ccm ambazo hazipo katika kitabu cha orodha ya wanachama

.Kata ya Nshambya Bukoba Mjini na maeneo mengine ya mji wa Bukoba zoezi linaendelea ingawa kuna wanachama wachache sana katika vituo.

.Mgombea mmoja katika jimbo la Bukoba(jina lake nitalitaja baada ya kupiga kura)jana aligoma kusaini makubaliano ya kutaka kila mgombea kukubaliana na matokeo na kuwa tayari kumuunga mkono atakayepitishwa .

.Wilayani Karagwe wanachama bado hawaamini macho wao kukuta wagombea wawili maarufu Gosbert Blandes(mbunge wa sasa) na Karimu Amri ambao walidaiwa kujitoa majina yao hayamo katika orodha ya wanaotakiwa kupigiwa kura.Hivyo hao wanachama siyo wagombea,baadhi ya akina mama wamegoma kupiga kura baadhi ya maeneo kwa kukosekana wagomea hao.

Wagombea kwa kila Jimbo

Bukoba Mjini:
Wagombea ni
1:Balozi Khamis Kagasheki,
2:Bw.George Rubaiyuka,
3:Bw. Josephat Kaijage,
4:Bi.Elieth Projestus
5: Dr.Anathory Amani,
6:Bw.Philbert Katabazi,
7:Bw.Mujuni Katarahiya
8: Bi.Celestina Rwezaura.

BukobaVijijini
Wagombea ni
1:Bw.Jasson Rweikiza ,
2:Bw. Nazir Karamagi
3:BW.Nelson Itagasa.

Muleba Kaskazini
Wagombea ni
1: Charles Mwijage
2: Bw.Ambrose Nshala.

Muleba Kusini
Wagombea ni
1😛rofesa Anna Tibaijuka,
2😀r Adam Nyaruhuma,
3:Bw.Stivin Tumaini,
4:Bw.Flavius Kahyoza,
5:Mhandisi Buruani Rubanzibwa,
6:Muhaji Bushako
7:Kaino Mendesi
8: Bw. Erick.

Jimbo la Ngara
Wagombea ni
1:Syprian Gwassa,
2😀r Philemon Rugumiliza,
3:Bi.Helen Adrian n
4:Bw.Wilbald Ede
5: Bw.Alex Gashaza,
6:Bw.Jelard Muhile,
7:Johakim Nchunda ,
8:Bw.Issa Samma
9: Bw.Ladslaus Bambanza.

Jimbo la Nkenge
Wagombea
1:Asumpta Mshama,
2😀iodorous Kamala,
3😀r Mazima,
4:Bw Frolent Kyombo,
5:Bw Julius Rugemalira
6:Bw......

Jimbo la Kyerwa
Wagombea ni .Innocent Seba Bilakwate,Stephano Edward Katemba
3.Lameck Chacha Ng'ang'a
4.Norbeth Kobwino
5.Sinsibath Kashunju Runyogote
6.Pancrace Shwekelela
7.Awaam Ahamada Ngalinda

Jimbo la Karagwe.
1.Mwalimu Dagobati Deogratias
2.Audax Christian Rukonge
3.Innocent Luga Bashungwa
4.Gosbert Begumisa Blandes
5.Alfred Rujwahuka
6.Amoni Chakushemeire Eustad
7.Karimu Amri

 
Tupe update byabato, vipi aliyekuwa mbunge wa nkenge nasikia anatoa mitusi tu.
 
mwambieni tibaijuka asijisumbue coz akipita kura za maon ukawa tutamiliki jimbo saa asubuh, eti na issa samma anagombea jimbo la ngara vs gashaza, yetu macho but be care record inaelekea kuvunjwa kwa mara ya kwanza ngara kuongozwa na upinzani
 
Kamanda Byabato asante. Kina bwana mmoja anaitwa Daniel kule Kyerwa mbona hujamtaja,INA maana kajitoa, au anatumia kina lingine.? Tunaomba na update za madiwani, has a Kara ya Mabira Kyle Kyerwa.
 
Kamanda Byabato asante. Kina bwana mmoja anaitwa Daniel kule Kyerwa mbona hujamtaja,INA maana kajitoa, au anatumia kina lingine.? Tunaomba na update za madiwani, has a Kara ya Mabira Kyle Kyerwa.

Majina tumeyapata kutoka kwa katibu wa CCM wa wilaya,nitafuatilia tena kujua kama hilo jina lipo au la.
matokeo ya wagombea udiwani mkoa mzima nitayapata kama kawaida,sema ni vigumu kuyaweka humu yote.kwa kata ya mabira nitakupatia.
 
Mbona sijaona Biharamulo? Au ccm hawajaweka wagombea
 
Ingependeza Mods wangebadili title ili iwe Kura za maoni ccm Nchi nzima na si kwa kina nshomile peke yake.

Ni vigumu mimi kuleta live updates za kila jimbo nchini.Wakinazisha hiyo thread sawa lakini mimi naleta mahali nilipo basi.

Pili hilo neno kwenye nyekundu siku hizi ni tusi,hivyo tambua hapa umetukana na kama we ni muungwana iwe mara yako ya mwisho kutumia neno hilo.Ubarikiwe
 
na Tibaijuka yumo jamani! Ati na Rugemalila! Ngoja tuone kama Tibaijuka na rugemalila watampitisha huko vikao vya juu! Si walimkata Lowasa kwa kigezo cha maadili???
 
Tunakushukuru kwa updates zako Mr. Mathias Byabato, tupo tayari kusikiliza hizo sarakasi za ccm. najua leo watu wataumizana na kupelekana Hospitali, je madokta wamejiandaa vipi kupokea majeruhi wataoumiza kwenye kura za komediani ccm. CCM leo inamwaga damu kwenye kura za maoni watatifuana mbaya mno..
 

Roger that....Nafuta kauli ya red.
 
.Wanachama wa CCM wanaendelea na upigaji kura ingawa katika maeneo mbalimbali ya kata ya Kanyigo wilyani Missenyi wasimamizi wanalalamikia kuwepo kadi za ccm ambazo hazipo katika kitabu cha orodha ya wanachama.

.Kata ya Nshambya Bukoba Mjini na maeneo mengine ya mji wa Bukoba zoezi linaendelea ingawa kuna wanachama wachache sana katika vituo.

.Mgombea mmoja katika jimbo la Bukoba(jina lake nitalitaja baada ya kupiga kura)jana aligoma kusaini makubaliano ya kutaka kila mgombea kukubaliana na matokeo na kuwa tayari kumuunga mkono atakayepitishwa .

.Wilayani Karagwe wanachama bado hawaamini macho wao kukuta wagombea wawili maarufu Gosbert Blandes(mbunge wa sasa) na Karimu Amri ambao walidaiwa kujitoa majina yao hayamo katika orodha ya wanaotakiwa kupigiwa kura.Hivyo hao wanachama siyo wagombea,baadhi ya akina mama wamegoma kupiga kura baadhi ya maeneo kwa kukosekana wagomea hao.
 

Sarakasi zainaanza, madokta wawetayari kupokea waliopasuliwa, hiyo ndio ccm bila ya rushwa na wizi haichaguliki.
 
Baada ya Leo ndio tutajua ugumu au urahisi wa kazi walionayo ma-campaigner wa ukawa na ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…