Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Toyota na kampuni za Ulaya na Marekani wamechelewa sana kwenye EV

Mchina kwa sasa anatawala kwenye EV
Nchi za EU wameweka Sheria ngumu zaidi Kwa magari ya china yasitawale soko Lao la ndani maana wanajua hawatakuwa na ishu tena kwa magari Yao..
Ufaransa wamefuta ushuru wa kuingiza magari ya umeme lkn Kwa magari ya china ni ngumu kuingiza ufaransa Hadi ukanunulie Spain na Italy ndipo uingize ufaransa.

Mchina ni balaa Kwa dunia yote
 
Ni kweli

Tatizo wao wanamzuia Mchina, halafu yeye Mchina anazidi kuteka soko la mataifa mengine mfano Latin America, South East Asia na Ulaya Mashariki

BYD wamefungua kiwanda Hungary

Chery wamefungua Thailand

Chery wana mpango wa kufungua kiwanda Spain

BYD nao wana mpango wa kufungua kiwanda Mexico

Umeona mchezo unavyoenda
 
Chery ni balaa hii kampuni Wana ndinga zinatisha
 
Xiaomi’s factory produces 40 electric cars every hour — or, one car in 76 seconds — without a single human worker.

View attachment 2974804
Amazing..hawa jamaa wametuacha mbali sana sijui nchi zetu zitawezaje kufika kwenye tech kama hizi au hata kama upo mpango kwenda kwenye robotic manufacturing
 
Volkswagen tena.
Wapenzi wa Volkswagen wametuletea Volkswagen ID.Concept ambayo ni Smart Car.



Hii ni SUV flani, ambayo Volkswagen wamesema ina latest and most advanced Level 4 Automated driving.

PS: Automated Driving zina level kadhaa kuanzia level 1 hadi level 5. Hii Level 1 ni simple and lighter driving assistance mfano Cruise Control, Lane Keeping Assistant etc wakati Level 4 ni FSD (Full Self Driving) kwamba gari itafanya kila kitu kuanzia acceleration, braking, cornering, kusimama kwenye traffic lights, kupark, kusimama zebra, etc as long umeshaweka destination kwamb naenda Mbagala Rangi Tatu. Tuendelee na gari letu..

Hapa dereva ukiacha gari ijiendeshe, wewe na abiria wako wa mbele mnaweza geuka kabisa 180 degrees kupiga story na abiria wa nyuma. Sio kigeuza shingo, kugeuza seat kabisa.




Ukiwa unaendesha hii chuma afu uka engage "Center Pilot" hapa AI inatake over inaanza kuendesha yenyewe chuma. Kwanza mkwara unaanza steering wheel ambayo inashape yetu pendwa ila mbaya Yoke style inazama na kubakisha dashboard plain, kama kwenye Sci-fi movies.



Pia vioo vyote, cha mbele na vya pembeni, vina display information mbalimbali ambazo utaamua watu wa nje wazione au muzione nyie wa ndani tu.

Mfano, unaweza ukawa uko ndani unaendesha chuma afu unapita sehemu kuna mazingira mabaya, ukaamua kuweka display vioo vya pembeni vikawa vinaonesha wallpaper beach au kitu garden, ili passengers wafurahi.

Kioo cha mbele kina HUD augmented reality down to earth projection, nadhani hii tumeona kwenye Mercedes Benz EQS yaan HUD hii unakua unaona kabisa as if vitu vimewekwa kwa chini. Nashindwa kuelezea ila ngoja angalia hii picha kama itakusaidia.



Na mwisho kuna hygiene mode, ambayo uta engage mfano umetoka safari afu ulikua na familia. Gari chafu kwa ndani. Basi mkishuka, uka enable gari itahakikisha ndani hakuna mtu afu itatoa UV light na antibacteria filters zitasafisha hewa ya ndani na kuna vacuum cleaner anaitwa Lupo ataanza kusafisha ndani kuondoa takataka ndogo ndogo.


Ilikua moja ya presentation nzuri tungeweka link hapa ya video ila haina maana vitajaa vilink sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…