Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Mercedes Benz G Class ya Umeme.

If you can't beat them.. G Wagon ya umeme iyooo ikiwa na range ya kilometa 570 kwa full charge moja.

Hii ni series ya tatu ya Magari ya umeme kutoka Mercedes Benz baada ya EQ series (EQS, EQB, EQCE, EQA etc) na Mercedes-AMG GT 63 S E (ina E Performance/Hybrid).
 
Jaecoo J7 kutoka kwa Chery
Jaecoo ni sub brand ya Chery (kama Lexus na Toyota) ambayo specifically ni kwa magari nje ya China. Sasa wametoa Hybrid moja kali sana, J7.

Hii SUV, itakayo anzwa kuuzwa huu mwaka itakua approximately $50,000/= tu. Hii ina engine 1.6L Turbo na battery. Ina produce horsepower 194 na ukiwek EV peke yake ina range ya 100km.



Ndani kuna screen ya inch 10 Instrument Panel (screen ya dereva ya kuonesha speed, gear, na info nyingine) na kuna screen ya inch 15 pale katikati.

Pia gari ina level 2 ADAS yenye adaptive cruise control, automatic braking system, lane departure warning, blind spot detection.
 
Chery tena waja na T1 na T5 SUV
Chery tena wazindua SUV mbili kwaajili ya off-road. T1 na T5.

T1 ni hybrid SUV yenye 1.5L engine.

T5 pia ni Hybrid SUV yenye engine 2.0L ambayo ukiweka full tank na full charge inaenda kilometa 1400.
 
Amazing..hawa jamaa wametuacha mbali sana sijui nchi zetu zitawezaje kufika kwenye tech kama hizi au hata kama upo mpango kwenda kwenye robotic manufacturing
Sisi tumewekeza sana kwenye siasa za maji taka

Now China uses more robots in factories than the rest of the world combined.



Angalia gap hilo
 
BYD, XIAOMI au kampuni yoyote ya magari ije pia iwekeze Tanzania aisee. Dah Xiaomi mbaya sana kwenye EV yaani najua kabisa Elon Musk kila akilala lazima aote gari za Xiaomi zikiwa zina mkimbiza 😂
Huenda watengenezaji wa Chinese trucks & buses wakatangulia kufikiria kuwekeza Afrika Mashariki na kati maana kwa sasa wameliteka soko
 
Marekani wameshikwa pabaya na China

Ndani ya mwezi huu Marekani imewatuma wajumbe 2 waende China ziara tofauti

Janet Yellen (US Treasury Secretary)
Antony Blinken (US Secretary of State)

Wote katika ajenda zao mojawapo ya ajenda yao wanailalamikia China kuwa inachofanya sasa ni industrial overcapacity ikitia ndani kwenye utengenezaji wa EV

Wamesahau kuwa China imewekeza sana kwenye industrial robot na autonomous AI-based driving system
 
Sipati picha hili gari likitumika huku bongo na hawa bodaboda itakuaje!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…