Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Hadi mifugo washazizoea kunusa na kulala chini yake, so siyo deal tena kwa washua labda kina sisi huku pangu pakavu πŸ˜‚!.

Niulize swali; hiyo gari inaunguruma kama hizi za mafuta hama inakuwaje?.
EV's zote ni zero noise yaani hapa ni mwendo kama upo chumbani Tu.
Haya magari utapata mlio kutokea kwenye matairi Tu
 
Mercedes Benz wazindua E Class mpya
Yes, E Class za aina mbili, 6 cylinders 3.0L Turbo na 4 cylinders 2.0L Turbo zinakuja, utachagua diesel au petrol.

Kwa ndani itakua na super screen kama kwenye EQS, screen ya dereva itakua na 12.2 inch na screen ya pale kati 14.4 inch.

Kwa shape wanasema itakua ndefu (kubwa) kidogo kuliko model ya E Class iliyopo sokoni sahivi.
 
Chery wafukuzwe aisee.

Chery__wamezindua Exeed E08 ambayo ni Luxury MPV (Multi Purpose Vehicle). Hii chuma ni ya umeme (EV) tunategemea itawaficha wakina Alphard mitaani.

View attachment 2975959View attachment 2975960
πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
Barabara zijengwe sasa chuma kama hii kuizamisha kwenye tope au kuipandisha upande upande kwenye tuta sio haki kabisa
 
Yuanhang wazindua EV Luxury Sedan Y7
Vita ya Mchina kumuangisha Elon Musk inaendelea. Je Model 3 sedan ataweza shindana na chuma kama hii?

Hawa Yuanhang mwaka jana walizindua Y6 na sasa kwenye Beijing Auto Show wamwtuletea hii sleeky looking Y7.



Pale kati kwenye cockpit kuna 17 inch infotainment screen na HUD & augmented reality ya 70 inch (sijakosea, inch 70).

Kama una penda music hii gari ina amplifier 19, na seat za nyuma kila mtu ana screen yake na anaweza akacontrol baadhi ya vitu kwenye screen yake mwenyewe.

Kuhusu power bado hawajaweka hewani ila range inakadiliwa kua 800km.
 
Watumie tumie nasi tuanze kudaka vyuma hivi used miaka ya mbeleni.

Saa hizi mzigo unasomaje?
 
Mchina kama ameweza kuitoa Scania na magari mengine Kwa nchi za Africa na Asia tutegemee kuwatoa tena kwenye magari ya UMEME.
Hawa jamaa sio watu wa michezo kama wajapan
 
Ora 3 kutoka Great Wall Motors
Ora 3 aka Good Cat yazinduliwa ikiwa na bei ya $14,000 na range ya kilometa 400.

Gari ina panoramic sunroof, ADAS Level 2, ikija na AI autonomous parking, cruise assist, traffic jam assist.


Ndani tuna dual screen, ya upande wa dereva kuna 7 inch LCD screen na infotainment kuna 10 inch screen.
 
Nasikia Bwana Elon Musk yupo China, kaenda kwa issues mbili, moja kuendesha gari ya Xiaomi (SU7) na pili, kuongea na serikali ya China kuhusu kuruhusiwa FSD - Supervised (Full Self Driving Supervised).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…