Updates za kifo cha Afande Luteni Kanali Muna aliyeuawa Kawe kwa kuchomwa kisu na dereva bajaji Kato

Hapo polisi walicheza kama Pele, saivi ingekuwa Kato naye ashaagwa tayari
 
Maisha ya cheo yanakutaka uongozwe sana na hekima na kujitambua huku ukiwa mwepesi wa kuelewa mazingira kwamba wapi utumie cheo chako wapi usikitumie.

Kwa case ya huyu marehemu unaweza ukaona huyu alinyimwa vitu hivi ndiyo maana cheo chake (sizungumzii hicho kipya alichokuwa anaenda kukitumikia bali chochote alichokuwa nacho) kimekuwa mlango wa kumuondoa duniani,hauwezi ukaambiwa tu sogeza gari halafu ukaanza kupiga watu wazima wenzako makofi huo ni ulimbukeni.
 
Kama maelezo ya mtoa hoja ni ya ukweli, huyu mwanajeshi aliyeuawa ni katili, mshenzi na ilibidi afufuliwe ili afunguliwe mashitaka, ahukumiwe ndio afe tena,mwanajeshi HANA HAKI YA KUPIGA RAIA, hii ni vigilante,kangaroo court, zote hizi sio utamaduni wetu, bila shaka huyu mwanajeshi ni mzulu wa kwa mashu, maana kule kuna violence people's walioifanya SA kuwa violent nation, bodaboda afunguliwe docket na kuhukumiwa kutokana na ushahidi sio mihemko, nani kakupa madaraka ya kupiga raia, huu ni ukenges
 
Mkewe na mwanae wakiwa ndani daah, soo Sad..,R.I.P Afande!!
Kwa mwanaume anayejitambua hapo palikuwa siyo pakuonyesha ubabe,ukiwa na familia epuka sana shari huyo unayemletea shari anaweza kuwa yupo vizuri kuliko wewe ukaumbuka mbele ya mkeo na wanao.

Tuachane na kumuua tu-assume kwamba Bajaj driver Kato angekuwa yupo vizuri kurusha mkono akampasua hiyo familia yake ingemuonaje?mkewe wangepishana kauli siku amwambie mwanaume gani wewe unajifanya una mafunzo ya kijeshi unapigwa na dereva wa Bajaj asiyejua hata kushika bastola?bado angethubutu kusema mkewe ana dharau?maana hayo angekuwa ameyataka yeye.
 
Kama Kila raia anaekutana na ubabae wa askari polisi na jeshi angekua anajichukulia hatua mikononi namna hiyo pengine Kila wiki wangekua wanazikwa askari sio chini ya 100,
mtuhumiwa tayali ameshikwa wanapiga watu ili iweje 🤔🤔 wanadhani ndio watu watawaogopa🤔kama Wana nguvu Sana waende kupigana vita Ukraine na Israel huko wanahitaji nguvu kazi🤔 si ushamba huo🤔🤔 haya ni moja ya madhara ya kujaza la saba na waliopata ziro kidato nne kwenye jeshi
 
Asante kwa taarifa
 
Wanasema alikuwa amepata kidogo!
 

Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…