updates za UDOM


Usitetee kitu ambacho kiko uchi namna hiyo, mimi najua swala la rushwa kwa ajira za UDOM tangu nilipohudhuria usaili mwaka jana. palikuwa na watu zaidi ya 3000. Nafahamu jamaa yangu mmoja aliyeombwa rushwa na akatoa huku majina ya watu waliofaulu oral interview yakichakachuliwa na kuingizwa ya wale waliofaulu kupata connection ya kuhonga. Jamaa yangu mwingine alipambana sana ili apate kuhonga alishindwa maana hakuwa na connection, walimuogopa.

Kama yalifanyika mwaka jana kwa nini isiwezekane mwaka huu.

Tena nilisikia mkipokea pesa mnachomoa baadhi ya viambatanisho (nakala za vyeti) vya wenye sifa ili wapoteze sifa na watu wenu wapite. Kwendra huko
 
Hili liko wazi. Last year nilipata connection na nikatakiwa nitoe kitu kidogo. Roho yangu ilisita. na nilikosa nafasi. Yule mwenzangu alonipa inshu hiyo ya kitu kidogo akala shavu. This time nikajipanga ki kitu kidogo but unfortunate nimeambiwa na mdau kwa nafasi niloomba kila siku msururu wa waheshimiwa wakiwa wameandamana na watoto zao wanafurika administration kuweka mambo sawa. Kidau changu nikidogo hivo hakitaweza fanikisha. kwani hata hivo kati ya nafasi zile kumi za post yangu tayari kuna watu sita wako fixed na hao wanaoendelea kumiminika kwa ofc nahisi nishaikosa hata kabla sijaitwa kwenye intavyuu. Hiyo ni kweli wadau.
 
nchi kweli ishauzwa kama na ajira zinauzwa huu kweli ni ujinga serikali iko wapi au iko rikizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…