LGE2024 UPDP, Demokrasia Makini wazindua kampeni

LGE2024 UPDP, Demokrasia Makini wazindua kampeni

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa zikiwa zinakaribia ukingoni, viongozi wa vyama vya siasa nchini wameendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kwa amani na utulivu kwenye uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa United Peoples Democratic Party (UPDP), Twalib Kabeje, amezindua kampeni za chama hicho kitaifa mkoani Mwanza leo Novemba 25, akiwataka wananchi kuwachagua viongozi waliosimamishwa na UPDP kwa ahadi ya kuleta mabadiliko chanya katika mitaa yao, yakiwemo maji safi, barabara bora na siasa safi.

Wakati huohuo, Chama cha Demokrasia Makini pia kimezindua rasmi kampeni zake leo jijini Mwanza, kupitia mwenyekiti wake wa kitaifa, Costa Kibonde. Kibonde amewanadi wagombea wa chama hicho na kuwaahidi wananchi maendeleo iwapo watawachagua katika mitaa mbalimbali nchini.

Wagombea wa vyama hivyo wameendelea kusisitiza umuhimu wa kupiga kura kwa amani, huku wakionya dhidi ya vurugu zozote siku ya uchaguzi.

 
Vyama vyenye mipango hivyo,
Unazindua kampuni na kuzifunga siku hiyo hiyo dah 🐒
 
Back
Top Bottom