Upekee wako utathaminika tu ukiupeleka mahali panapohitajika

Upekee wako utathaminika tu ukiupeleka mahali panapohitajika

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Mzee mmoja, tumwite Hekima, aliamua kumpa kijana wake gari lake la miaka mingi baada ya kuhitimu masomo ya Chuo Kikuu.

Kabla ya kumkabidhi, alimtaka alipeleke kwa watu tofauti ili kujua thamani yake halisi kwa wakati huo.

Gari lenyewe ni Volkswagen Beetle, na alishalitumia kwa zaidi ya miaka hamsini.

Dogo alipolipeleka kwa wauzaji wa magari mitumba, aliambiwa atapewa $10,000 kwa kuwa limeshatembea maili nyingi sana.

Hakuridhika, akalipeleka kwenye ofisi inayokopesha hela, akaambiwa atalipwa $1,000 kwa sababu lina umri mkubwa.

Mwishoni, alilipeleka kwenye club ya wamiliki wa magari yanayofanana. Wahusika walikuwa tayari kumpa $100,000 kwa sababu ni moja ya magari adimu sana.

Somo: kama huthaminiki ulipo, inawezekana siyo sehemu sahihi kwako.

Kwa hisanani ya Quora
 

Attachments

  • Screenshot_20240915-120859.jpg
    Screenshot_20240915-120859.jpg
    245.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom