BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Diwani wa Kata ya Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Salome Mnyawi amesema hivi sasa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya tanzanite wanapekuliwa kwa staha tofauti na awali walipokuwa wakivuliwa nguo, kabla ya Wabunge kupinga upekuzi wa aina hiyo.
Mnyawi ameyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wilayani hapa.
Mnyawi amesema awali wanawake na wanaume walikuwa wanavuliwa nguo ili kupekuliwa wanapopita kwenye lango, ila baada ya wabunge kukemea hilo wanapekuliwa kwa staha.
"Tunawapongeza wabunge kwa kusimama kidete kukemea hilo kwani halikuwa jambo jema kupekua kwa kudhalilisha ila hivi sasa upekuzi ni wa stara," amesema.