SoC01 Upelelezi ukiwa mbovu, hata uendesheji wake wa mashtaka utakuwa mbovu

Stories of Change - 2021 Competition

Fortunatus Buyobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
463
Reaction score
1,127
Nianze kwa kurejea maneno ya waheshimiwa majaji katika kesi ya rufaa No. 175 ya Mwaka 2010 ya JUSTINE KAKURU KASUSURA VS REPUBLIC ambapo majaji walisema hivi “Kwa heshima zote tunapenda kusema,kesi hii ilipelelezwa vibaya,hivyo iliendeshwa vibaya”.Kwa kauli hii utagundua, upelelezi ukiwa mbovu, hata uendesheji wake wa mashtaka utakuwa mbovu na hivyo ni rahisi kwa mshtakiwa kushinda kesi hata kama ni kweli ametenda kosa.

Najielekeza kwenye mambo ambayo mpelelezi makini anapaswa kuzingatia wakati wa upelelezi kama nitakavyoainisha hapa chini;

Uitikiaji wa taarifa ya tukio;Si kawaida kwa mpelelezi kuwepo eneo la tukio wakati tukio linatokea. Mashuuda au waanga wa tukio ndio hutoa taarifa polisi baada ya tukio. Inatakiwa afisa wa polisi kusikiliza kwa makini taarifa hizo ili kubaini tukio linaangukia kwenye mizani ipi (ujambazi wa kutumia silaha,kuvunja na kuiba,mauaji na mengineyo). Taarifa hizi zitamsaidia mpelelezi kujua nyenzo anayotakiwa kuambatana nazo tukioni.

Wapelelezi huenda eneo la tukio bila nyenzo muhimu kama vile futi kamba na kamera ambavyo vitamsaidia kuchora ramani ya eneo la tukio au kupiga picha.

Kwenye kesi ya rufaa namba 453 ya mwaka 2017 ya JOHN MADATA VS REPUBLIC, Mahakama ilibaini upande wa jamuhuri haukuchora ramani ya eneo la tukio katika kesi ya Kuvunja na kuiba. Mahakama ilisema angalau ramani ingekuwepo,ingeweza kuunganishwa na ushaidi wa utambuzi wa macho ambao mlinzi aliiambia mahakama kuwa alimtambua mshtakiwa. Majaji walizingatia,kwa kuwa ulikuwa ni usiku,tena ikiwa ni mara ya kwanza kwa mlinzi kumuona mshtakiwa,ramani ndio ingetoa utata ule wa utambuzi kwani ingeonyesha umbali kati ya taa kama chanzo cha nuru, na eneo alilokuwepo mtambuzi na mshtakiwa. Ushaidi wa utambuzi wa macho ingawa ulikuwa mzito, ukatupiliwa mbali kwa kosa dogo tu la mpelelezi kuitikia eneo la tukio bila nyenzo za uchoraji wa ramani ya eneo la tukio au walau picha ya eneo la tukio.

(Picha kwa hisani ya mtandao)
ezChUCvdxk_3yR5pPHQHqf1KPBMrQ6SQCCwN3XqqlqaAG8g8Br3Zj-2H7P1HzMEKsgmxBPzjtsghKILhhtK7DClMXuLYEmX9lEVRC3P8-7UBEiMjLkg0t1892enVP8GX2FKnwus=s0

Usafi wa eneo la tukio;Inatakiwa kuzungushia uzio eneo la tukio ili kuzuia wasiohusika kuingia kwenye eneo hilo na kutibua ushaidi na vielelezo. Pia maafisa wapelelezi wanapaswa kuvaa gloves wakati wakigusa au kuchukua vielelezo.Gloves zitazuia alama za vidole kubaki katika vielelezo. Watu wengi hujitetea kwa makosa wayafanyayo wapelelezi katika hili,kwani utetezi unaweza kuhoji inawezekanaje mshtakiwa akamatwe kwa kielelezo cha damu wakati hata mpelelezi alishuudiwa akiwa na damu siku ya tukio? Mfano juu ya hili ni kwenye kesi maarufu kama “Mauaji ya MUGARANJABHO” ya mkoani Mara mwaka 2010.

(Picha kwa hisani ya mtandao)
a5AgPneBU1fJXbYZpmMFeeA5w1h4OrURwtGmk4ZVDdH1YRZCPZbo5pVYSDIcG-MrZKJv_jjNeiWYzRrehGw0TbGpQi5GezpXdWx465wN7HyhE0SQWkkq9bjU6DTdtIcyswBNtF8=s0

Kuambatana na mtaalamu wa uchunguzi eneo la tukio;Mpelelezi aambatane na mtaalamu aliyebobea kwenye maswala ya uchunguzi wa kisayansi(Medical Forensic Expert).Kwa mfano tukio linahusu mauaji,wataalamu husaidia kuchunguza sampuli kama sumu,vilevi, madawa,matapishi na kilichomo tumboni mwa maiti.Pia mtaalamu anaweza kukadiria muda wa tangu kifo kimetokea hadi maiti ilipogunduliwa kwa njia ya “postmortem interval”(PMI).Mtaalamu hukagua maiti kwa kurejea hatua ambazo hupitia tangu kifo mpaka hali inayokutwa nayo.Hatua hizo ni Kupoteza nuru(Pallor-Mortis), Kushuka kwa joto la maiti(Algor-Mortis), Kukakamaa(Rigor-Mortis),ngozi kubadirika rangi(Livor-Mortisi),kuharibika kwa mwili (Putrefaction) na uwepo wa wadudu kama funza au nzi.Taarifa hizi ni muhimu kiupelelezi hivyo mtaalamu huyu anahitajika sana kuambatana na mpelelezi kwenye eneo la tukio.

Mahakamani huwa kuna utetezi waAlibi ambapo mshtakiwa hukana kuwa hakuwepo eneo la tukio wakati kifo kinatokea.Taarifa hii ya kitaalamu(postmortem interval),husaidia kuuangusha utetezi huu.

Usafirishaji wa vielelezo kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara; Kwa ajili ya uchunguzi,mara nyingi vielelezo hupelekwa kwenye ofisi ya mkemia mkuu wa serikali.Lazima sampuli zitunzwe kwenye vyombo visivyoathiriwa na mwanga, hewa na joto ili kusafirishia sampuli mpaka ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali. Ukosefu wa vyombo hivi husababisha sampuli kuharibika hivyo kutotoa matokeo yanayotarajiwa na hivyo kuathiri ujenzi wa kesi.

Kuunganisha kielelezo na ushaidi; Kama kesi ni ya mauaji,mpelelezi anawajibika kuhusisha kielelezo cha silaha iliyotumika na eneo la tukio. Kama mpelelezi amekuta maiti imechomwa kisu au imekatwa mapanga, ana wajibu mkubwa wa kuhakikisha anahusisha silaha iliyotumika na damu ya marehemu. Nikirejea kesi ya jinai namba 117 ya mwaka 2002 ya REPUBLIC Vs VECENT FLAVIAN MBAGA and others,Mwenyekiti wa kijiji cha LUKOBE na askari mgambo wa kijiji,walimkamata mtuhumiwa na kumsindikiza kwenda kituo cha polisi Morogoro,wakiwa wamebeba mapanga. Mtuhumiwa hakufikishwa lakini yake iliokotwa ikiwa na majeraha ya mapanga. Watu hawa walishitakiwa kwa mauaji na moja ya hoja ya Jamhuri ilikuwa ni marehemu kukutwa majeraha ya mapanga ikiwahusisha washtakiwa kuwa na mapanga siku ya tukio. Utetezi uliipangua hoja hii kwa kuwa hakukuwa na ushaidi unaounganisha mapanga ya watuhumiwa na damu ya marehemu. Washtakiwa hawakukutwa na hatia.

(Picha kwa hisani ya mtandao)
DwbzjNpEpoSkN7DCMF1P9uTEdbR9MMj9Y_aBJT8aBA83OresF-kzQNge6z--9C2_ty4iDgT4on1DNAg0UlLwiFY-8079BFGBgYfs4CwnLKNL030O4yeVrYyXLxs_f2CztvAwa20=s0

Makabidhiano ya vielelezo (Chain of custody); Vidhibiti vinapaswa kukabidhiwa kwa kufuata utaratibu wa sheria kuanzia eneo la tukio mpaka vinapofika mahakamani. Utaratibu huu usipozingatiwa hutoa mianya ya utetezi. Nikirejea kesi ya jinai namba 21 ya Mwaka 2018 ya REPUBLIC Vs DEOGRATIAS JACOB MSEMWA,maiti ya SHOLASTIKA NUNGU ilikutwa katika kijiji cha Muungano Zomba mkoani Songea. Juu ya maiti kulikuwa na daftari lililokutwa limeandikwa “Mimi Deogratius Msemwa nimemuua hawala wangu kwa sababu ametoa siri kwa mmewe kuwa nimezaa naye mtoto mmoja”.DEOGRATIAS akakamatwa akaambiwa aandike upya maneno kama yale.Daftari pamoja na maneno mapya ya DEOGRATIAS vikapelekwa Mbeya kwa mtaalamu wa maandishi Insp. JORAM MAGOVA. Mtaalamu huyu akathibitisha kuwa mwandiko wa Deogratias ndio uliomo kwenye daftari. Pamoja na ushaidi huu,kwa kuwa hakukuwa na nyaraka za “chain of custody”, ushaidi huu ulitupwa.Utetezi ulitaka kujua daftari lilitokaje kwenye tukio songea, likaenda Mbeya hadi kufika mahakamani.

Kumjaribu shaidi kabla hajapanda kizimbani(Voir dire); VOIR DIRE humaanisha kumpima shaidi kama anafaa kulingana na sheria ya ushaidi, kutoa ushaidi. Hii hufanywa mahakamani hasa kwa mfano shaidi akiwa ni mtoto mdogo kulingana na sheria ya ushaidi, kuona kama anaweza kukubalika kama shaidi. Wapelelezi wasisubiri hili likafanyikie mahakamani na kujikuta mashaidi wao wanakuwa "impeached". Wanapaswa kuwachuja mashaidi kwa kuzingatia mambo yafuatayo;

  1. Je wanajikanganya(inconsistent) kwenye ushaidi wao? Kitendo cha shaidi kujikanganya, kunaweza kusababisha shaidi akawa HOSTILE WITNESS yaani shaidi atoaye ushaidi usiomsaidia yule atolewaye ushaidi au sana sana kumuangamiza(Kwa upande wa mashtaka ni kupoteza kesi). Pia ni lazima kuhakikisha mashaidi wote wanatoa ushaidi usiokinzana kama wote wanaongelea mazingira sawa ya tukio. Kwa mfano Kuna shaidi anaweza sema kamuona muuaji na Panga huku mwingine akisema kamuona na Sime. Utofauti huu wa maelezo ni tatizo.
  2. Utambuzi; kama upande wa mashtaka utakuwa una shaidi wa macho, ni lazima kuhakikisha “Eyewitness” anakidhi vigezo vya kisheria vilivyomfanya akamtambua mshtakiwa wakati anatenda tukio.Vigezo hivyo ni;chanzo cha nuru kilichomsaidia kumuona mshtakiwa,muda aliotumia kumtizama mshtakiwa akitenda kosa,umbali kati yake na mshitakiwa na kama alimfahamu mshtakiwa kabla ya tukio? Katika kesi ya jinai namba 27 ya Mwaka 2018 ya REPUBLIC Vs ABDALAH BAKARI MKWINDA kuna mama( Bi ASIA) alichinjwa,mwane ndiye alikuwa shaidi wa macho aliyedai alimsikia mama yake akibishana na baba yake wa kufikia, lakini alijichanganya aliposema tochi ya “solar” ndio ilimsaidia utambuzi na baadae akasema ni mwanga wa mbalamwezi. Kwa Kigezo hiki kidogo tu,ushaidi huu ukatupwa. Kama shaidi wa macho ni mara yake ya kwanza kumuona mtuhumiwa siku ya tukio,ni muhimu shaidi huyu ashiriki gwaride la utambuzi kabla ya kumtambua mtuhumiwa kizimbani. Kwenye kesi niliyoitaja juu ya JOHN MADATA Vs REPUBLIC kuna ushaidi ulitupiliwa mbali kwa sababu walimtambua mshtakiwa mahakani bila kushiriki gwaride la utambuzi wakati ilikuwa ni mara yao ya kwanza kumuona mshtakiwa siku ya tukio.
  3. Kwa ushaidi wa kimazingira,ni muhimu sana wapelelezi wajenge ushaidi ambao hautoi nafasi ya mahakama kumhisi mtu mwingine nje ya anayetuhumiwa kuwa ndiye aliyetenda kosa.Kwa kimombo ni "The Inference drawn should be irresistible and shouldn't point to any one else but the accused". Kwa kimombo tena ni kwamba, "The inference drawn should be Incapable of more than one interpretation" Kusiwe na adithi zaidi ya moja hivyo kuleta hisia,mtu mwingine ndiye katenda na si mshtakiwa. Kwenye kesi ya LUKOBE Morogoro niliyoitaja juu,Wasindikizaji walituhumiwa kwa mauaji,lakini zikajengwa hoja Je haiwezekani mtu yule akawa ameuwawa na wananchi wenye hasira?Hoja hii iliwanasua washitakiwa. Wapelelezi wanatakiwa kuyahepuka maswali haya kwa kutengeneza mtiririko wa ushaidi unaoegamia kwa mtuhumiwa tu.
Matumizi ya nguvu katika upelelezi; Wapelelezi wanatakiwa kuacha uvivu wa kufanya upelelezi na badala yake kutumia nguvu kuwatesa watuhumiwa kuandika Maelezo ya Onyo na ungamo wakiwalazimisha kukili makosa. Mtuhumiwa hutekeleza matakwa ya mpelelezi atumiaye nguvu lakini mahakamani akakana ungamo lake. Ungamo lililokanwa na anayedaiwa kulitoa(repudiated confession) halina nguvu ya kisheria.Mahakama inaweza kutupilia mbali maungamo na maelezo ya onyo ikijiridhisha yalipatikana bila hiyari.

Kusoma na kuielewa ripoti ya Kitaalamu; Mpelelezi akae na mtaalamu ili amfafanulie aliyoyaandika kitaalamu kwenye ripoti yake. Akiielewa ripoti,ahakikishe kilichomo kwenye ripoti,kinarandana na ushaidi wa mashaidi aliowawaandaa. Kwa mfano daktari akiandika chanzo cha kifo ni “Strangulation”,mpelelezi aelewe Strangulation ni kuzibwa kwa njia ya hewa kwa kutumia mikono na sio kunyongwa. kunyongwa ni kuzibwa kwa njia ya hewa kwa kutumia nyenzo kama vile kamba.Makosa ya kushindwa kuielewa ripoti,huibua hoja za kiutetezi mahakamani.

(Picha kwa hisani ya mtandao)
6P2uIC5f1aBZL_Ao0l947_8MmEn1ImPfs3jQH_QhAXeppuk3EDSdwa3luJEDDRQiJoDkmJE9JQSTI7cd7kIzwqAGBcKFA1mBqi46op7bOfcYd53wjWQVeNCpos4KlssOH1bsGjA=s0

Ninahitimisha kwa kuwataka wapelelezi kufatilia makosa ya kisheria yanayosababisha kushindwa kesi mahakamani ili makosa hayo yasijirudie kwenye kesi mpya. Pia naamini darasa hili dogo litaweza kuwasaidia wasomaji,ikitokea bahati mbaya wameangukia kwenye kesi za jinai.

Wasiliana na mwandishi 0788916060
 
Upvote 42
Nawaomba sana michango yenu kwenye hii thread.

Pia naomba kura zenu kwenye uzi wangu huu. Kama unatumia simu chini kabisa ya uzi wangu niliopost utaona namba fanya kubonyeza mara moja tu hapo kwenye namba utakuwa umemaliza kunipigia kura. Kwa watumiaji wa kompyuta juu kabisa ya uzi kushoto utaona sehemu ya VOTE ukibonyeza utakuwa umefanikiwa kunipigia kura.
 
Kitufe cha kura sikioni
 
16th vote Environmental Security
 
Back
Top Bottom