Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili watu 13, wakihusishwa na uharibifu wa noti zenye thamani ya Sh4.6 bilioni, bado unaendelea.
Kesi hiyo, ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa muda mrefu, ilitajwa leo Alhamisi, Februari 20, 2025, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kwa mujibu wa mashtaka, kundi hilo linakabiliwa na makosa matano, mojawapo likiwa ni kuharibu noti hizo na kusababisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupata hasara kubwa.
Wakili wa Serikali, Winiwa Kasala, ameeleza kuwa upelelezi upo katika hatua za mwisho, lakini shauri limeahirishwa hadi Machi 20, 2025, kwa sababu Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Anna Magutu, yupo likizo.
Miongoni mwa washtakiwa ni wafanyakazi wa BoT waliotajwa kuwa Mariagoreth Kunzugala (maarufu kama Bonge), Henry Mbowe (Mzee wa Vichwa), Asha Sekiboko, Cecilia Mpande, Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo, na Mwanaheri Omary—wote wakiwa wakazi wa Dar es Salaam.
Washtakiwa wengine, ambao si watumishi wa BoT, ni Alistides Genand, Musa Chengula, Zaituni Chihipo, na Respicius Rutabilwa.
Hati ya mashtaka inaeleza kuwa kati ya Januari 2017 na Septemba 30, 2019, baadhi ya watuhumiwa, wakitumia nyadhifa zao ndani ya BoT, walivunja majukumu yao ya kazi na kuruhusu kutokea kwa kosa la kuongoza genge la kihalifu. Pia, Genand, Chengula, Chihipo, na wenzao wanadaiwa kushirikiana na watumishi hao wa BoT kurahisisha njama hizo.
Kosa lingine linalowakabili ni kuharibu noti 460,000 za Sh10,000 kila moja, zenye thamani ya Sh4.6 bilioni, kwa kuzikatakata. Pia, wanadaiwa kufaidika na Sh1.5 bilioni kutoka BoT baada ya kuwasilisha noti hizo benki hiyo.
Awali, walikuwa na mashitaka sita, lakini Juni 18, 2021, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliondoa shtaka la utakatishaji fedha, na kuwaacha na makosa matano yanayoendelea kushughulikiwa mahakamani.
Source: Mwananchi