Upendeleo, ushikaji ndio vinatumika kupeana uteuzi Awamu ya Rais Samia

Upendeleo, ushikaji ndio vinatumika kupeana uteuzi Awamu ya Rais Samia

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Ukiwa mdadisi na mwenye msimamo wa kisiasa wa kutetea maslahi ya umma utaona mwelekeo usiyoridhisha kuhusu teuzi za mama.

Utaona leo kina sabaya, Ally Hapi, na Makonda wote mama kawatupa nje. Tena sabaya akataka kumfunga kwa kesi ya kubumba. Badala yake wale waliyokua wamefumwa wakionesha chuki na kumpinga mtetezi wa umma JPM na kisha yeye kuwatema ndio wako kwenye usukani.

Na hata pale wamebainika kukoroga kazi kwa kuweka maslahi yao kwenye shughuli za umma bado anawahifadhi huku akiendelea kutowapa uteuzi vijana machachari watetezi wa umma kina makonda na sabaya na akiwa amemtema Ally Hapi huku akionekana kutetea maslahi ya umma vikali.

Cha ajabu Maharage rafiki yake januari mama anahangaika kuhakikisha anapewa shirika kubwa la umma baada ya kukoroga kuongoza tanesco huku ikiwa ameondolewa mtu mwenye weledi mkubwa halafu anaweka mirija yake anaharibu. La ajabu anataka kupewa shirika lingine kubwa TTCL watu wanapiga kelele mama mwenyewe anasema amegundua maharage ana biashara na ttcl japo haisemi. Kisha maharage anawekwa posta huku CEO wa posta mwenye record yake nzuri anawekwa benchi.

Huu mwenendo wa wapigaji kuwa na nguvu kuwekwa kwenye taasisi kubwa za umma lazima ukome. Ukiona jinsi watu matajiri wala hawana ujuzi ila uzoefu wa upigaji wanawekwa kwenye bodi za wakurugenzi inastaajabisha.

Ingefaa bodi za wakurugenzi na u ceo wa mashirika makubwa ya kama tanesco, TRC, TTCL na mengine nafasi na sifa zinazotakiwa zitangaziwe watanzania wote kisha majina ya wenye kufuzu ndio mamlaka ya uteuzi zipelekwe kwa vetting kabla ya uteuzi.
 
Usisahau pia kwamba mwenye nacho huongezewa, asiye nacho hunyang'anywa hata kidogo alicho nacho.
 
kumpinga mtetezi wa umma jpm
Mxiuuuuu! Mtetezi wa umma!!!? Huyu mpuuzi ndiyo ameiharibu nchi hii kw taarifa yako. Alikuwa mkabila, mkanda, mporaji, muuaji, mtekaji na mpiga risasi.

Mama ana madhaifu ktk uongozi lkn kamwe usimlinganishe na huyu shetani amabye hakustahili hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji.
 
Back
Top Bottom